loader
Dstv Habarileo  Mobile
TPA
Picha

Old Trafford kuchukua mashabiki 23,500

KLABU ya Manchester United imeamua kuubadili Uwanja wa Old Trafford na kuchukua watazamaji 23,500 ili kuwezesha watu kukaa kwa nafasi, na imesema kuwa “imefadhaika” kwa mashabiki kuzuiwa kuingia viwanjani.

Serikali ilipendekeza kuwa watu taratibu waruhusiwe kuingia uwanjani kuanzia mwanzoni mwa Oktoba, lakini ilibadilisha kauli yake kufuatia kulipuka tena kwa virusi vya corona.

"Tulipokea maelekezo ya serikali, “alisema Collette Roche, muendeshaji mkuu wa Klabu ya Man United. "Nashawishika kusema kuwa tutaweza kuwaweka mashabiki kwa usalama zaidi.”

Mwezi uliopita, Waziri Mkuu Boris Johnson alisema mazuio mapya yataendelea kutumika hata miezi ijayo.

Athari za mlipuko wa janga la corona kwa kiasi kikubwa limeathiri michezo na timu, ikiwemo klabu ya United ambayo imejikuta ikipata hasara ya kiasi cha Pauni milioni 70 mapato yaliyotarajiwa katika kipindi cha kuanzia Juni 30, 2020 ikiwa ni matokeo ya moja kwa moja.

"Tulitumia karibu miezi miwili tukifanyia kazi maelekezo ya serikali ili kutekeleza michakato sahihi ili kuhakikisha tunakuwa karibu na watu 23,500 katika uwanja huu ili kuhakikisha watu wanakaa kwa nafasi," alisema Roche.

Aliongeza kuwa mipango ya United imefanywa wakati muafaka kwa mashabiki na kupimwa joto kabla ya kuingia kutapunguza hatari.

Mechi za Ligi Kuu zimekuwa zikionekana bure kupitia katika chaneli za kulipia, lakini tangu wakati huo utata wa zaidi ya Pauni milioni 14.95 malipo kwa kila anayeangalia yalianzishwa kwa baadhi ya mechi.

Mashabiki wanagomea mechi hizi ambazo zilikusanya zaidi ya Pauni milioni 300,000 kwa ajili ya msaada.

BARCELONA wamethibitisha kuwa wameafikiana na ...

foto
Mwandishi: MANCHESTER, England

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi