loader
Dstv Habarileo  Mobile
Vodacom yatangaza kulipa bilioni 427.5 gawio kwa wanahisa

Vodacom yatangaza kulipa bilioni 427.5 gawio kwa wanahisa

KAMPUNI ya Vodacom Tanzania imetangaza kuwa mwaka huu kampuni hiyo italipa jumla ya Sh bilioni 427.5 kama gawio kwa wanahisa wake, ambapo kati ya hizo, Shi bilioni 400 ni gawio maalum na Sh bilioni 27.5  ni gawio la mwisho wa mwaka wa fedha ulioishia  Machi 31, 2020.

Aidha katika mwaka wa fedha uliopita (2019/2020), kampuni hiyo ilirekodi ukuaji wa mapato ya huduma ambayo kwa kiasi kikubwa yalisababishwa na huduma za internet (data) iliyoingiza Sh bilioni 180.8 (asilimia 9.8) pamoja na matumizi ya huduma ya M-Pesa yaliyochangia Sh bilioni  358.2

Akizungumza katika Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Vodacom mapema leo Ijumaa, Mwenyekiti wa Mpito wa Bodi ya Wakurugenzi wa Vodacom, Margaret Ikongo ameelezea matumaini juu ya utendaji wa kampuni hiyo licha ya huduma kuzuiwa kwa zaidi ya wateja milioni 2.9 kulingana na mahitaji ya usajili wa alama za vidole kwa kutumia kitambulisho cha Taifa (NIDA).

"Licha ya mwaka huu kuwa wenye changamoto nyingi katika ushindani mkali wa soko pamoja na mazingira ya udhibiti, kampuni ilirekodi uendeshaji wenye mafanikio ulioletwa na kasi ya kibiashara iliyoanza mwaka wa fedha uliotangulia.

“…tuliwekeza jumla ya shilingi bilioni 154.6 katika mtandao wetu pamoja na miundombinu ya teknolojia ya habari ili kuhakikisha wateja wananufaika na huduma bora na mtandao unaopatikana kote nchini. Matokeo yake ni kwamba tumedumisha mapato ya wateja na uongozi wa hisa, na kufikia jumla ya wateja milioni 15.5 wa matumizi ya sauti, data na ujumbe mfupi (sms) na wateja milioni 10.1 wa M-Pesa,” amesema Ikongo.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Hisham Hendi amesema kuwa sababu ya matokeo mazuri ya kampuni hiyo ni kufanikisha utekelezaji wa mikakati yake vizuri

"Katika mwaka wa fedha uliopita, matumizi ya data yaliongezeka kwa asilima 14.6, na ukuaji mkubwa ulikuja kutokana na matumizi ya 4G. Hii inaonyesha mahitaji makubwa ya huduma za data kupitia simu za mkononi na pia inathibitisha nia yetu katika kuongeza huduma mbalimbali za data kwa wateja kupitia uwekezaji endelevu katika miundombinu ya mtandao, hii ni pamoja na kuleta simu janja za bei nafuu sokoni lakini pia utoaji wa huduma ya data za bei rahisi, "amesema Hendi.

Mkurugenzi huyo ameongeza kuwa mazingira ya biashara yanabaki kuwa na ushindani mkubwa, na kwamba wamejidhatiti katika kutoa huduma bora kwa wateja kupitia ubunifu wa kidijitali pamoja na ujumuishwaji wa kifedha.

Katika Mkutano huo Mkuu wa Mwaka, Jaji (Mstaafu) Thomas Mihayo alijiunga na kampuni hiyo iliyoorodheshwa katika soko la hisa la Dar es salaam kama mkurugenzi huru. Wanahisa pia walichagua wakurugenzi mbalimbali wapya pamoja na kuwapitisha wakurugenzi waliokuwepo katika bodi ya kampuni hiyo.

 

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/23df83d68660144f416b5988fe7cf587.JPG

MKURUGENZI wa Idara ya Diplomasia ya ...

foto
Mwandishi: Alfred Lasteck

1 Comments

  • avatar
    Alex
    16/11/2020

    Voda kwa kweli mnatuibia haiwesekan mtu unaunga kivurush cha wiki Halafu unapewa dakika 80 za kupiga mchana halafu unapewa dakika 150 za kupiga saa sita usiku. Je inamaana Mtu Kama una mke wako au faliaa kwa ujumla Ni ujasiri gani hiyo ambayo mtu unaamka saa sita za usiku na kupiga cm kama c mnatuletea shida

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi