loader
Dstv Habarileo  Mobile
TPA
Picha

Wazee 6,000 wapewa kadi za bima za CHF

MKUU wa Mkoa wa Arusha, Iddi Kimanta amewakabidhi wazee zaidi ya 6,000 kadi za bima za CHF zitakazowawezesha kupata huduma za matibabu.

Akizungumza katika hafla ya kukabidhi kadi hizo, Kimanta alisema kadi hizo zitawapunguzia  unafuu wa maisha na kuwasaidia kutibiwa kwa urahisi bila gharama yoyote.

Alisema jiji la Arusha limefanya jambo la muhimu la kuwathamini wazee kwa kuwapatia kadi hizo za matibabu, zitakazowawezesha kupata huduma za afya wanapopata maradhi.

“Unajua mzee hana garantini ya kuumwa, saa yoyote anaumwa, hivyo kwa kupata kadi hiyo itawasaidia sana kupunguza gharama za matibabu yao, unaweza kukuta mzee anatumia hata shilingi 400,000 kwa mwezi kwa ajili ya kujitibu,” alibainisha Kimanta.

Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, Rebeka Mongi alisema jiji hilo limetenga Sh milioni 41 kwa mwaka wa fedha 2020/2012 kwa ajili ya kuwalipia  wazee bima za afya.

Wakati huo huo, Mganga Mkuu wa Jiji la Arusha, Dk Kheri Kagya alisema wamechukua hatua hiyo ya kuwapatia kadi wazee hao, baada ya kubaini changamoto mbalimbali zinazowakabili. Alisema kadi hizo za bima ya afya zitawasaidia kutibiwa hadi hospitali za rufaa.

Awali akisoma risala kwa Mkuu wa Mkoa, Katibu wa Baraza la Wazee Jiji la Arusha, Kasimu Seramu alitaja baadhi ya changamoto wanazokumbana nazo ni ukosefu wa madaktari maalum kwa ajili ya kuwahudumia wazee. Changamoto nyingine ni hospitali nyingi zina madirisha ya wazee, lakini hazina wauguzi kwa ajili ya wazee. Changamoto nyingine ni ukosefu wa dawa kwa ajili ya magonjwa yasiyoambukiza yanayowakumba wazee na ukosefu wa uwakilishi katika taasisi za juu.

Alisema kwamba kwa sasa wameanza kujipanga kuunda baraza la wazee la taifa na wanatarajia kufanya uchaguzi wao Novemba 15, mwaka huu na kupata viongozi wa kuwasemea kitaifa.

MGOGORO uliobuka ndani ya ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Maalum, Arusha

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi