loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Masauti akana kutoka na Tanasha

MSANII wa muziki kutoka Kenya Mohamed Said ‘Masauti’ amesema ukaribu wake na nyota Tanasha Donna ni wa kikazi na sio kwamba wanatoka kimapenzi.

Hivi karibuni msanii huyo aliyezaliwa Mombasa Kenya alihusishwa kutoka kimapenzi na Tanasha, ambaye ni mpenzi wa zamani na mzazi mwenzake, Nassibu Abdul ‘Diamond Plutnumz’.

Masauti aliyeko Dar es Salaam kwa ajili ya kujitangaza alipohojiwa na moja ya Radio kubwa nchini alisema kuna kazi walishirikiana kuandika mashairi na kuimba pamoja kwa hiyo ule ukaribu wao watu wakamaanisha kitu ambacho sio kweli.

“Tulishirikiana kuandika nyimbo lakini suala la mahusiano halipo, sisi ni mrafiki kwasababu kwanza yule ni msichana wa kule namuheshimu,”alisema.

Msanii huyo waliimba wimbo wa pamoja na Tanasha unaoitwa ‘Liar’ aliomshirikisha Tanasha ambao ulifanya vizuri baada ya kupokelewa na mashabiki wengi wa ukanda wa Afrika Mashariki.

MANCHESTER United leo itaikaribisha Liverpool katika ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi