loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wadada wampa tabu Alikiba

NYOTA mkongwe wa muziki wa kizazi kipya Alikiba ameelezea changamoto anazokutana nazo katika muziki hasa pale anapowashirikisha wadada katika video zake hupata wakati mgumu.

Katika mahojiano na Mseto East Afrika kinachorushwa na Citizen ya Kenya, alisema pale anapokuwa katika matendo na kuwashika video vixen humsababishia lawama kutoka kwa mke wake.

Alisema licha ya mke wake kulalamika au kuuliza maswali mengi juu ya wadada hao anaofanya nao kazi, bado  anajua ni kazi yake ni lazima afanye hivyo, ingawa na yeye hana nafasi ya kujiachia tena kama zamani kwasababu ameoa.

“Mke wangu lazima alalamike na kusema kidogo hiyo yote ni kuonesha mapenzi. Kuna muda ni lazima nitamshika mdada ila siwezi kwenda mbali kwasababu nina mke,”alisema.

Katika hatua nyingine, msanii huyo alitaja sababu zilizokuwa zinachangia kushindwa kutoa nyimbo mara kwa mara ni kwa kuwa alitaka anapotoa wimbo mmoja ukae muda na kuwa na thamani kuweza kurudisha fedha alizotumia.

Alisema kutoa mara kwa mara nyimbo kunaua nyingine ambazo amezitoa lakini baadhi ya wasanii miaka hii wameharibu utaratibu huo wa zamani.

GWIJI wa muziki wa Bongo Fleva ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi