loader
Dstv Habarileo  Mobile
TPA
Picha

JPM KUAPISHWA NOVEMBER 5, HAKUNA SHEREHE

RAIS Mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Magufuli ataapishwa rasmi kushika dola kwa awamu ya pili Novemba 5, mwaka huu 2020.

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi, Hamphrey Polepole aliwashukuru watanzania na wapiga kura kwa kumchagua kwa kura nyingi Rais Mteule, John Magufuli ambaye kesho atapokea hati ya uteuzi jijini Dodoma.

Amesema katika hafla hiyo ya kupokea hati, CCM itakuwa na wawakilishi wasiozidi 400 kwa sababu kuwa chama hicho kinajinasibu kwenye kauli mbiu ya hapa kazi tu na kuwa sherehe itaandaliwa mwishoni mwa mwaka 2025.

“Tunawashukuru watanzania,wapiga kura kwa kumpa mgombea urais wa CCM kura za kishindo, tunasema kwetu mmetuamini tunaahidi kazi na kesho kwenye hafla ya kukabidhiwa hati ya uteuzi tutakuwa na idadi ndogo ya watu 400 tu, kwetu sherehe tutafanya mwishoni mwa mwaka 2025, tukimaliza kazi ‘’,amsema Polepole.

 

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi