loader
Dstv Habarileo  Mobile
TPA
Picha

CCM yataka wateule wote kuanza kazi mara moja

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Humphrey Polepole amesema kuwa wateule wote waliopata nafasi ya uongozi katika uchaguzi mkuu waanze kazi mara moja kuandaa utaratibu wa kufuatilia kero za wananchi.

Polepole amesema hayo muda mfupi uliopita katika ofisi ndogo ya chama hicho iliyopo Lumumba jijini Dar es Salaam na kubainisha kuwa wateule wanatakiwa kuchapa kazi kwa kuwa  viongozi wa chama watakuwa wakali ili waweze kusimamia ipasavyo maslahi mapana ya nchi hasa kipindi hiki taifa linapopambana kufanya mapinduzi makubwa ya kiuchumi.

Amesema kuwa Rais Mteule Magufuli pamoja na kushinda uchaguzi bado anaendelea kuchapa kazi ndio maana  muda akiongea na wanahabari alikuwa kazini akishuhudia utuaji wa ndege kubwa kwa mara ya kwanza katika Uwanja wa Ndege Dodoma  baada ya kufanyiwa maboresho.

Katika hatua nyingine Polepole amesema kuwa  Novemba 05, kwenye Uwanja wa Jamuhuri jijini Dodoma kutakuwa na tukio la Rais Mteule Magufuli  kuapishwa rasmi huku kwa upande wa Zanzibar Rais mteule wa visiwa hivyo DK Hussein Mwinyi  anategemea kuapishwa siku ya Jumatatu wiki ijayo.

Amesema kuwa hapo kesho   Rais Mteule Magufuli  anategemea kupokea hati ya ushindi wa uchaguzi jijini Dodoma ambapo kwa mwaka huu amesema kutakuwa hakuna sherehe kama ilivyozoeleka na badala yake wataudhuria watu wasiozidi mia nne.

Aidha, Polepole aliwapongeza viongozi wa dini kwa namna walivyokuwa mstari wa mbele kuhubiri amani kipindi chote cha uchaguzi jambo lililosaidia tukio hilo kumalizika kwa amani.

foto
Mwandishi: Alfred Lukonge

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi