loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Kampeni zanoga Marekani

WASHINGTON, Marekani

MGOMBEA Urais kwa tiketi ya Democratic Joe Biden yupo Michigan wakati Mgombea wa Republican Rais Donald Trump yupo Pennsylvania wakiendesha kampeni  katika maeneo hayo muhimu yanayoweza kuwasaidia kupata ushindi katika uchaguzi mkuu utakaofanyika kesho.

Katika kampeni za Biden aliungana Rais Mstaafu Barack Obama ambaye alisisitiza kuwa ni wakati wa Marekani kuachana na matukio na vurugu za uongozi wa Trump.

Hata hivyo, Rais Trump alisema kuwa kutakuwa na wimbi kubwa la ushindi kwa chama chake kuliko inavyotarajiwa.

Katika kura za maoni zinazoendelea Biden amekuwa akiongoza jambo ambalo hata hivyo inabidi liongezewe nguvu na ushindi katika baadhi ya majimbo muhimu.

Zaidi ya watu milioni 85 wamepiga kura mapema katika uchaguzi nchini humo, kati yao milioni 55 wamepiga kura nje ya vituo vyao na kufanya uchaguzi huo kuwa na idadi kubwa ya watu waliopigakura kwa kipindi cha muda mrefu.

Biden na Trump walifanya kampeni katika mji huo wa Michigan kabla ya kwenda mji wa Detroit ambako waliungana na mwanamuzi Stevie Wonder. Katika uchaguzi wa mwaka 2016, Trump alishinda kwa kura chache kutoka Michigan.

Katika kampeni hizo mwanamuziki Wonder aliubadili wimbo wake wa Superstition na kuweka mashairi yanayomzungumzia Biden na Mgombea Mwenza wake Kamala Harris.

Kwa upande wa Biden akizungumza katika maeneo kadhaa jijini humo, alimshambulia mpinzani wake Trump na kueleza kuwa ni wakati sasa wa kufungasha virago na kwenda nyumbani wake.

“Tumechoshwa na vurugu, ujumbe wa twitter wa kila mara, hasira, kushindwa na mtu kukataa kuwajibika,” alisema.

Kwa upande wake, Trump kwenye mikutano yake ya hadhara jijini Pennsylvania alitumia kauli mbiu ya minne zaidi na kuelezea kuwa uhuru wa Marekani ulianza tangu miaka minne iliyopita ni wakati wa kumalizia kazi hiyo.

WANACHAMA wa Chama cha Republican nchini ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi