loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Washambuliaji waua 19 chuo kikuu

WATU wenye silaha wamevamia Chuo Kikuu cha Kabul na kuua wanafunzi katika vyumba vyao vya madarasa huku kuwashambulia wengine wakati wakikimbia. 

Shambulio hilo la Jumatatu ni la pili dhidi ya taasisi ya elimu jijini hapo kwa zaidi ya wiki moja.

Washambuliaji hao watatu waliwaua watu wasiopungua 19, wakiwemo wanafunzi kabla ya vikosi vya usalama vya Afghanistan kuwapiga risasi watu hao wenye silaha. 

Picha zilizotolewa na ofisa mwandamizi wa serikali zilionesha maiti za wanafunzi zikiwa sakafuni ndani ya madarasa, wengine karibu na vitabu vyao. Mwanafunzi mmoja alionekana kupigwa risasi alipokuwa akikimbia kupitia dirishani.

"Walikuwa wakimpiga risasi kila mwanafunzi waliyemwona hata waliwapiga risasi wanafunzi waliokuwa wakikimbia," shuhuda Fathullah Moradi aliliambia Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC).

Taliban walisema wapiganaji wao hawakuhusika katika shambulio hilo na hakuna kikundi kingine kilichodai kuhusika mara moja.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani, Tariq Arian, alisema watu 19 waliuawa na wengine 22 kujeruhiwa kabla ya huduma za usalama kumaliza shambulio hilo.

"Hili ni shambulio la pili kwa taasisi za elimu huko Kabul. Watoto na vijana wa Afghanistan wanahitaji kujisikia salama kwenda shule," Mwakilishi Mwandamizi Raia wa NATO nchini Afghanistan Stefano Pontecorvo, alisema katika taarifa.

Jimbo la Kiislamu, bila kutoa ushahidi lilidai kuhusika na shambulio la kujitoa mhanga lililoua watu 24 wakiwemo wanafunzi wa kituo cha elimu huko Kabul, Oktoba 24.

Vurugu zimeikumba Afghanistan wakati serikali na mazungumzo ya Taliban yakiwa yanaendelea huko, Qatar kujaribu kusuluhisha makubaliano ya amani, wakati huo Marekani  ikirudisha nyumbani wanajeshi wake.

WANACHAMA wa Chama cha Republican nchini ...

foto
Mwandishi: KABUL, Afghanistan

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi