loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wamarekani wapigakura kuchagua rais

WAMAREKANI wamepiga kura kumchagua rais atakayeongoza taifa hilo kwa kipindi cha miaka minne ijayo. Aidha ni wakati wao wa kuamua endapo Rais Donald Trump atabaki katika Ikulu hiyo ama la.

Trump ambaye pia ni Rais wa chama cha Republican anapingwa na mteule wa Chama cha Demokratic Joe Biden, anayejulikana kama Makamu wa Rais wa Barack Obama, lakini amekuwa kwenye siasa za Marekani tangu miaka ya 1970.

Siku ya uchaguzi inapokaribia, kampuni za kupigia kura zinajaribu kupima hali ya taifa kwa kuuliza wapigakura ni mgombea yupi wanapendelea apate nafasi ya kuongoza taifa hilo lenye nguvu duniani.

Kura za kitaifa ni mwongozo mzuri wa jinsi mgombea anavyopendwa nchini kote kwa jumla, lakini siyo njia nzuri ya kutabiri matokeo ya uchaguzi ingawa Biden anaongoza kwa kura za kitaifa za urais.

Uchaguzi wa mwaka 2016, Hillary Clinton aliongoza kura na akashinda karibu kura milioni tatu zaidi ya Donald Trump, lakini bado alishindwa, hiyo ni kwa sababu Marekani hutumia mfumo wa vyuo vya uchaguzi, kwa hivyo kushinda kura nyingi siyo kila wakati kushinda uchaguzi mkuu.

Kwa mujibu wa shirika la habari la BBC, licha ya tahadhari hiyo, Biden amekuwa mbele ya Donald Trump katika kura nyingi za kitaifa tangu mwanzoni mwa mwaka huu. Katika miezi ya hivi karibuni, amezunguka karibu asilimia 50 na mara kadhaa amekuwa akiongoza kwa alama 10.

Taarifa ya BBC jana ilisema zaidi ya watu milioni 98 wamepiga kura za mapema, na kuashiria kuwa ni uchaguzi ambao idadi kubwa zaidi kushiriki kuwahi kutokea katika kipindi cha karne moja 

Katika uchaguzi wa Marekani, wapigakura huchagua katika ngazi ya majimbo kuliko uchaguzi wa jumla wa kitaifa.

Kuchaguliwa kuwa rais, mgombea anapaswa kushinda takribani kura 270 katika uchaguzi wa mapema kila jimbo nchini Marekani hupata kura fulani kutegemea na idadi ya watu ndani ya jimbo na kuna jumla ya kura 538 za kunyakua.

Mfumo huu unaeleza ni kwa namna gani inavyowezekana kwa mgombea kushinda kwa kura nyingi kwa ngazi ya taifa- kama Hillary Clinton alivyofanya mwaka 2016-lakini bado alipoteza katika uchaguzi huo.

WANACHAMA wa Chama cha Republican nchini ...

foto
Mwandishi: WASHINGTON, Marekani

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi