loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Putin asisitiza rasimu ya mkakati kufikia malengo

RAIS wa Urusi, Vladimir Putin ametoa msisitizo juu ya kukamilishwa kwa Rasimu ya Mpango Mkakati, utakaoisaidia nchi hiyo kufikia malengo yake ya maendeleo.

“Hii ni hatua muhimu katika kazi yetu," alisema Putin akiwa katika mkutano na wajumbe wa Baraza la Mawaziri na kuongeza kuwa anatarajia watendaji wote watafanya juhudi kuhakikisha wanautekeleza mpango mkakati huo.

Baada ya kuripoti kuwa uandishi wa mpango wa pamoja wa kufikia malengo ya maendeleo ya kitaifa kupitia 2024 na kipindi kilichopangwa hadi 2030 umekamilika, Waziri Mkuu, Mikhail Mishustin alibainisha kuwa mashauriano yote yanayohitajika na wafanyabiashara, wataalamu na wabunge, yalifanyika wakati waraka huo ukitayarishwa.

Mikhail alisisitiza kuwa baada ya hatua hiyo, sasa rasimu ya mpango huo itawasilishwa kwa rais.

"Tuko tayari kuiwasilisha kwenye mkutano wa Baraza la Rais juu ya maendeleo ya kimkakati na miradi ya kitaifa kama ilivyoombwa," alisema Waziri Mkuu. 

WANACHAMA wa Chama cha Republican nchini ...

foto
Mwandishi: MOSCOW, Urusi

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi