loader
Dstv Habarileo  Mobile
TPA
Picha

Wananchi EAC wachangamkie fursa ya masoko ya kikanda

DESEMBA mwaka huu ujenzi wa soko la ukanda wa Afrika Mashariki katika mpaka wa Tanzania na Uganda, Mutukula wilayani Kyotera unatarajiwa kuanza.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Rural United Business Association Network (RUSBA) Ltd, Karim Karamagi alisema hivi karibuni kuwa soko hilo la kikanda litajengwa katika Kijiji cha Kasanvu kwenye Barabara ya  Kyotera- Mutukula na kuwa ujenzi wa soko hilo umesubiriwa kwa muda mrefu.

Ameeleza kuwa ujenzi wake umefadhiliwa na Kampuni ya Afrika Kusini ya Degitech Energy Company Ltd litajengwa kwa Sh za Uganda trilioni 2.8 huku likikamilika litakutanisha wenye viwanda, wauzaji wa jumla, wasambazaji na wateja kutoka nchi za EAC.

Karamagi anasema soko hilo litakuwa likifanya kazi Jumanne na Ijumaa na pia litakuwa na uwanja wa kuhifadhi wanyama wakiwamo kondoo, mbuzi na ng'ombe watakaohifadhiwa kwa muda kwa ajili ya kuchinjwa na kuuza nyama kwenye masoko ya ndani na ya kimataifa.

Karamagi alisema walipata ekari 200 za ardhi zilizokodishwa kwao na Serikali ya Mtaa ya Wilaya ya Kyotera, na wana hakika miundombinu yote itajengwa huko.

Mutukula iko kusini mwa Wilaya ya Kyotera katika mpaka wa kimataifa kati ya Uganda na Tanzania takriban kilometa 225.1 kwa barabara kutoka Kampala.

Ni dhahiri kuwa ujenzi wa soko hilo ni hatua nyingine ya ufanyaji biashara kwa nchi za EAC hususan Tanzania na Uganda kwa kila wakati kupeleka bidhaa kwa wingi kwa ajili ya kuuza katika masoko mbalimbali ya ndani nan je ya nchi kama anavyoeleza Katibu Mtendaji wa Chama cha wafanyabiashara wenye viwanda na Kilimo nchini (TCCIA) mkoa wa Kagera Rwechungura Mali kuwa asilimia 70 ya chakula kwa nchi za Rwanda,Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo wanategemea Tanzania.

Hivyo ni vema wakati ujenzi huo ukianza kujengwa ,kuwepo kwa mikakati mbalimbali kwa wafanyabiashara na serikali kuhakikisha watanzania wanatumia fursa hiyo vizuri kwa wenyewe ambao kuna bidhaa nyingi kupeleka kwenye soko na siyo kuwaachia watu wan chi nyingine wanunue Tanzania na kupeleka kwenye soko hilo litakalokutanisha wafanyabiashara mbalimbali.

Ni dhahiri kuwa mara shughuli za biashara zikianza kwenye soko hilo,wahitaji wan chi nyingine ambazo siyo za EAC watafika kutafuta bidhaa hivyo watanzania wanatakiwa kuhakikisha kila bidhaa zinazohitajika kwa wingi katika soko hilo kutoka Tanzania zinapelekwa kwa wingi.

Lakini pia kwa bidhaa zinazohitajika nchini kutoka katika nchi mbalimbali za EAC ni vema wafanyabiashara kuingiza nchini kutoka katika soko hilo ili kwezesha wananchi kuzipata kwa gharama nafuu ukilinganisha na unafuu wa kodi kulingana na mtangamano wa jumuiya ya Afrika Mashariki.

Kuanzishwa kwa soko hilo nchini Uganda kunatoa fursa kwa nchi nyingine za EAC kuw ana masoko kama hayo kuwezehsa muingiliano wa bidhaa toka EAC kuwa nafuu na rahisi jambo litakalosaidia kuongeza ajira na kipato kwa wananchi wake na kila nchi kuongeza mapato kutokana na kuuza bidhaa,kuhudumia wafanyabiashara na nyinginezo.

foto
Mwandishi: Theopista Nsanzugwanko

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi