loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Chuo Kikuu cha Juba chapiga marufuku mikutano ya siasa

CHUO Kikuu cha Juba kimepiga marufuku mikutano ya kisiasa ndani ya chuo hicho kwani inasumbua wahadhiri na kuonya kuwasimamisha kazi au kuwaachisha kazi ambao hawatatii.

Taarifa ya chuo hicho imesema hatua ya kuzuia mikutano hiyo imechukuliwa kutokana na kusababisha changamoto kwenye taaluma na katika mkutano wa maseneta ilibainika kuwa siasa ni moja ya vyanzo vya machafuko ambayo yanatishia utulivu wa kitaaluma wa vyuo vikuu.

"Seneti iilibaini matatizo ya  kiwango cha juu yanayotokana na mikutano ya kisiasa, hivyo ili kukabiliana na hili mikutano ya kisiasa ikome mahali popote chuoni," ilisema taarifa hiyo.

Taarifa hiyo ilionya kuwa  mwanafunzi yeyote atakayekiuka agizo hilo  atasimamishwa au kufukuzwa katika chuo kikuu hicho.

Oktoba Mosi mwaka huu utawala wa chuo hicho uliwasimamisha masomo baadhi ya wanafunzi kutokana na kushiriki maandamano yaliyofanyika mwishoni mwa wiki hiyo.

Wiki iliyopita wanafunzi wa  Chuo Kikuu cha Juba walijitokeza barabarani kupinga masuala kadhaa yaliyowekwa na uongozi wa chuo hicho ikiwamo kuzuia kuingia madarasani ambao hawajalipa ada ya masomo.

Vikosi vya majeshi ya Uganda vimeondoka kwenye makazi ...

foto
Mwandishi:  JUBA

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi