loader
Dstv Habarileo  Mobile
TPA
Picha

Tarura yataka wafugaji kutunza barabara

WAKALA wa Barabara Vijijini na Mijini (Tarura) katika Wilaya ya Hanang’ mkoani Manyara, umewataka wananchi kutunza na kulinda miundombinu kwa kuacha kuchunga mifugo katika barabara zinazojengwa na kukarabatiwa kwa kuwa gharama za matengenezo hayo ni kubwa.

Aidha, Tarura imewataka wafugaji kutoruhusu mifugo yao kwenda umbali mrefu katika barabara mpya zinazofunguliwa na kukarabatiwa kwa kuwa hali hiyo husababisha uharibifu unaohitaji ujenzi wa barabara hizo kabla ya kukamilika.

Meneja Tarura katika Wilaya ya Hanang’, Nicolaus Ludigery alisema limekuwa ni tatizo sugu kwa baadhi ya wakazi wa wilaya hiyo kuharibu kwa makusudi barabara kwa wafugaji kutembeza mifugo umbali mrefu wa zaidi ya km 20 kufuata barabara.

"Hatuna shida sana na wafugaji wanaokatisha barabara na mifugo yao, bali wanaofuata barabara na kufanya uharibifu mkubwa; tunawashauri wafugaji kuacha tabia hiyo mara moja kwani wanaharibu mazingira na hawa ni sambamba na watu wanaolima kando ya barabara bila kujali sheria za kufuata zilizopo kuhusu barabara," alisema.

Alisema katika mwaka wa fedha wa 2019/, Wilaya ya Hanang’ imetenga asilimia 20 ya bajeti yake kuchonga barabara zenye urefu wa kilometa 31.28 na zitagharimu Sh milioni 158.32.

Barabara hizo ni za mji wa Katesh za kilometa 18 na barabara za Endasack - Sabilo zenye urefu wa kilomita 8.3 na barabara ya Nangwa- Gitin yenye urefu wa kilometa 4.4.

"Kati ya hizo barabara zilizo nje ya mji  wa Katesh zitakuwa na urefu wa kilometa 12.7 ambazo ni barabara za Endasack - Sabilo  yenye urefu wa kilometa 8.3 na barabara ya Nangwa- Gitin yenye urefu wa kilometa 4.4. Baraba hizo ni za kiwango cha udongo na changarawe na ziko katika utekelezaji wa Ilani ya CCM,” alieleza.

Kwa mujibu wa Ludigery, awali watu hao walikuwa wakifika hospitali kwa kuzunguka umbali mrefu wa takriban kilometa mbili hadi tatu, hivyo kufunguliwa kwa barabara hiyo kutafupisha mwendo huo hadi takriban kilometa moja ili kufika hospitalini hapo.

Kuhusu matengenezo ya maeneo korofi katika barabara hizo, alisema asilimia 98 ya barabara hizo ni maeneo korofi yaliyoharibiwa na mvua kuhitaji matengenezo, ujenzi wa jengo la ikulu ya wilaya hiyo pamoja na ujenzi wa mitaro ya maji.

Ludigery alisema mji wa Katesh uko chini ya mlima, hivyo mvua inaponyesha maji hujikusanya na kufurika katika mitaa hali inayosababisha kuwapo hitaji la mitaro ya maji.

foto
Mwandishi: Theddy Challe, Hanang’

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi