loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Lungu asisitiza muhogo kuongezewa thamani

RAIS Edgar Lungu wa Zambia amesema mradi wa kilimo, uzalishaji na uboreshaji unaoendelea katika Wilaya ya Chitambo ni mpango jumuishi wa kuongeza thamani.

Aliyasema hayo wakati wa ziara yake ya kikazi katika Jimbo la Kati kutembelea Mradi wa Kilimo, Uzalishaji na Uboreshaji wilayani humo.

Rais Lungu alisema mradi wa kiwanda cha kuchakata zao la muhogo utasaidia katika kuongeza thamani ya zao hilo.

Alisema serikali yake inahimiza suala la kuongeza thamani kwa mazao mbalimbali ili kutengeneza ajira.

“Jambo hili ni zuri, kuongeza thamani mazao ndiyo jambo tunalolitaka kama serikali, ndiyo njia ya kuifuata,” alisisitiza Rais Lungu.

Alisema wakulima wanapaswa kusaidiwa mbegu bora za mihogo kwa kuwa siyo mbegu zote zinazofaa katika kuongeza thamani ya zao hilo.

Ofisa Mratibu wa Kilimo wa Wilaya ya Chitamabo, Katumwa Mutandi, alisema kuwa wakulima wanaozalisha zao la muhogo wamebainisha namna wanavyonufaika na mradi huo.

Mutandi alisema kuwa kutokana na malighafi iliyopo kwa ajili ya mradi huo, wakulima tayari watakuwa na soko la uhakika kwa mradi huo unaotekelezwa.

 

 

 

PAPA Francis ameanza ziara yake ya ...

foto
Mwandishi: LUSAKA, Zambia

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi