RAIS wa Marekani Donald Trump amesema amemfukuza kazi mkuu wa usalama Shirika la Usalama wa Miundombinu ya Uchaguzi (Cisa), Chris Krebs ambaye alipingana na madai ya udanganyifu kwenye zoezi zima la upigaji kura.
Hadi sasa Rais huyo kutoka taifa hilo lenye nguvu kubwa ya kiuchumi duniani hajakubaliana na matokeo ya uchaguzi huo yaliyompa ushindi Joe Biden.
Wakati huohuo, mshindi wa kiti cha Urais Marekani, Joe Biden amekutana na washauri wake wa mambo ya usalama wa taifa kikao ambacho hakikuhusisha wataalam wa upelelezi kutoka serikalini.
Baadhi ya wabunge kutoka chama cha Trump, Republican, wamehimiza taarifa za ujasusi kuwasilishwa kwa Biden, kuelekea Januari 20 siku ambayo Rais huyo mteule ataapishwa.