loader
Dstv Habarileo  Mobile
Nimechoka kubeba  matatizo ya Barca- Messi

Nimechoka kubeba matatizo ya Barca- Messi

LIONEL Messi amesema amechoka kulaumiwa kwa matatizo ya Barcelona baada ya wakala wa zamani wa Antoine Griezmann kumshutumu.

Messi, 33, alikutana na kundi la waandishi wa habari kwenye uwanja wa ndege wa El Prat mjini Barcelona juzi akiwa anarejea kutoka kwenye majukumu ya kimataifa alipokuwa na timu ya taifa ya Argentina.

Aliulizwa maoni yake juu ya madai ya Eric Olhats kwamba amekuwa akifanya vizuri zaidi Barca na kushindwa kufanya hivyo kwa timu yake ya taifa.

"Nimechoka kuwa tatizo la kila kitu kinachoendelea kwenye hii klabu,” alisema Messi.

Griezmann mara zote amekuwa akisema kwamba uhusiano wake na Messi ni mzuri na vyanzo vya karibu na mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa vilisema imepita miaka mingi tangu alipozungumza na Olhats.

Wawili hao walikuwa na uelewano mzuri Barca katika mechi ya mwisho kabla ya kwenda mapumziko ya kimataifa ambapo Messi alimtengezea Griezmann bao.

Lakini kumekuwa na tetesi za hivi karibuni kwamba Messi anajipanga kuondoka Barca baada ua kumaliza mkataba wake mwishoni mwa msimu huu.

Mshambuliaji huyo wa Argentina alitaka kuondoka Agosti baada ya kufungwa mabao 8-2 na Bayern Munich huku vyanzo vya habari vikidai Manchester City inamtaka lakini Barca haikumruhusu kuondoka.

Akizungumza suala hilo, Messi ambaye amekuwa Barca kwa miaka 20, alisema shida yake kubwa ilikuwa ni Rais wa zamani Josep Maria Bartomeu na uongozi wake.

Lakini Bartomeu alijiuzulu Oktoba jambo lililotafsiriwa kwamba mbadala wake atafanya mazungumzo na Messi juu ya kusaini mkataba mpya.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/e02b73be79dd9b919487e913e8ae2b0b.jpg

“Jesse Lingard atajifunza kutokana na makosa yaliyowapa faida ...

foto
Mwandishi: BARCELONA, Hispania

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi