loader
Dstv Habarileo  Mobile
Ujerumani yadhalilishwa kimataifa

Ujerumani yadhalilishwa kimataifa

WINGA wa Manchester City, Ferran Torres amefunga ‘hat-trick’ yake ya kwanza kwenye maisha yake ya soka wakati Hispania ilipoidhalilisha Ujerumani kwa kuifunga mabao 6-0 kwenye michuano ya ligi ya kimataifa.

Matokeo hayo yanaifanya Hispania kuungana na Ufaransa kwenye timu nne zilizofuzu fainali ya michuano hiyo.

Katika mechi hiyo ya marudio ya fainali ya Euro 2008, mshambuliaji wa zamani wa Chelsea Alvaro Morata aliifungia Hispania bao la kwanza kabla Torres hajafunga la pili.

Rodri alifunga la tatu na Torres akaongeza la nne na la tano.

Mikel Oyarzabal akafunga bao la sita dakika ya 89.

Hispania na Ufaransa zitaungana na Ubelgiji na Uholanzi kucheza nusu fainali na baadae fainali za micuano hiyo.

Katika mechi hiyo, Hispania ilitawala kila idara na mabingwa hao wa zamani wa Kombe la Dunia Ujerumani wakiwa hawana mbinu zozote kuepuka aibu hiyo.

Ujerumani imeshinda mechi tatu kati ya nane mwaka huu,  ikifunga mabao 14 na kufungwa 17.

Katika mechi hiyo ilipaswa kuepuka kipigo ili ifuzu fainali.

Kocha wa Ujerumani, Joachim Low alipewa nafasi ya kujenga upya timu baada ya kuondolewa mapema kwenye fainali za Kombe la Dunia mwaka 2018.

Ikiwa inashika nafasi ya 13 kwenye ubora wa viwango duniani, kwa kiwango ilichoonyesha juzi ina kazi ya kufanya kabla ya kuanza mwaka mwingine wa michuano ya Ulaya.

Matokeo mengine ya mechi hizo Ubelgiji iliifunga Denmark mabao 4-2 Uholanzi iliifunga Poland mabao 2-1.

England iliifunga Iceland 4-0, Serbia ilishinda 5-0 dhidi ya Urusi, Wales ilishinda 3-1 dhidi ya Finland, Ufaransa iliifunga Sweden 4-2. Ureno ikiwa ugenini iliifunga Croatia 3-2.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/28760cab2e8089811969d627e01cb744.jpg

“Jesse Lingard atajifunza kutokana na makosa yaliyowapa faida ...

foto
Mwandishi: MADRID, Hispania

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi