loader
Dstv Habarileo  Mobile
TPA
Picha

Yanga yapania kufanya kweli

TIMU ya soka ya Yanga imepania kuendeleza ubora wake kwa kufanya vizuri katika michezo iliyoko mbele yao ili kukusanya pointi nyingi zitakazowasaidia kuwa karibu na taji la Ligi Kuu.

Kocha Msaidizi, Juma Mwambusi alisema Dar es Salaam jana kuwa vijana wake wana ari na morali ya kupambana kutimiza lengo walilojiwekea.

“Msimu huu hatutaki utani, tunajipanga kuendelea kukusanya pointi nyingi kadri siku zinavyokwenda zitakazotupa nafasi ya kuwa karibu na taji, naamini inawezekana tukiendelea kupambana,”alisema.

Alisema wakati kwenye mapambano ya kupigania taji, mashabiki wao wawe pamoja nao kuwaunga mkono katika safari ya kutafuta mafanikio na kutengeneza timu.

Mwambusi alisema pia, wamekuwa wakitafuta ufumbuzi katika safu yao ya ushambuliaji ambayo hupata wakati mgumu wa kufunga mabao na muda sio mrefu mambo yatakuwa mazuri.

Yanga inayoongozwa na Kocha Mkuu, Cedric Kaze, imekuwa katika mwenendo mzuri msimu huu ikionesha wazi haitaki utani.

Katika michezo 10 iliyocheza mpaka sasa imeshinda saba na kupata sare tatu ikiwa ndio timu pekee haijapoteza mchezo wowote ikishika nafasi ya pili kwa pointi 24 nyuma ya kinara Azam FC yenye pointi 25.

Mchezo ujao utakaochezwa keshokutwa itakutana na Namungo kwenye uwanja wa Benjamini Mkapa kabla ya kukutana katika mchezo mwingine wenye ushindani mkubwa dhidi ya kinara, Azam.

Rais wa Tanzania Dk John Magufuli ...

foto
Mwandishi: Grace Mkojera

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi