loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Prisons, Mtibwa kumekucha

LIGI Kuu mzunguko wa 11 inaendelea leo kwa timu ya Tanzania Prisons kushuka dimbani kuwakabili Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Nelson Mandela, Sumbawanga.

Prisons mchezo wake wa mwisho wa ligi kabla ya mapumziko ya kupisha michuano ya kimataifa, ilishinda bao 1-0 dhidi ya Ihefu.

Timu hiyo inashika nafasi ya nane kwa pointi 15 baada ya kucheza michezo 10, kushinda minne, kupata sare tatu na kupoteza mitatu.

Aidha, Mtibwa Sugar imetoka kupoteza dhidi ya Coastal Union bao 1-0 ikiwa nyumbani. Wakata miwa hao wa Manungu wanashika nafasi ya 12 kwa pointi 11, baada ya kucheza michezo 10, kushinda mitatu, sare mbili na kupoteza mitano.

Mchezo huo ni muhimu kwa kila mmoja kuhakikisha wanapambana na kupata pointi tatu.

Mchezo mwingine Dodoma Jiji itachuana dhidi ya Biashara United kwenye uwanja wa Jamhuri, Dodoma.

Huenda wenyeji hao wakamaliza hasira zao kwa Biashara baada ya mchezo wao uliopita kupoteza dhidi ya Azam FC mabao 3-0. Wageni wao wametoka kupata sare ya bao 1-1 dhidi ya KMC.

Biashara imekuwa bora msimu huu baada ya kucheza michezo 10, kushinda mitano, sare mbili na kupoteza mitatu ikishika nafasi ya nne kwa pointi 17.

Timu ya Dodoma imekuwa ikizidi kushuka tofauti na walivyoanza awali huenda ni kutokana na mwenendo wa matokeo yao. Wanashika nafasi ya 11 kwa pointi 12 baada ya kucheza michezo 10, kushinda mitatu, sare tatu na kupoteza minne.

Mchezo huo unaweza kuwa mgumu kwa pande zote mbili ila atakayepata matokeo mazuri ni yule aliyejiandaa dhidi ya mwenzake.

Kwa upande mwingine, Ruvu Shooting itakutana na Mbeya City kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Mchezo wa mwisho Ruvu imetoka kupata sare ya bao 1-1 dhidi ya Mwadui sawa na Mbeya City waliopata matokeo kama hayo dhidi ya Polisi Tanzania.

Ni mchezo mgumu unaohitaji matokeo hasa kwa wageni Mbeya City walioko katika nafasi ya pili kutoka mwisho kwa pointi saba katika michezo 10 waliyocheza. Ruvu iliyoko nafasi ya tano kwa pointi 16 wanahitaji matokeo kuendelea kuwa nafasi nzuri za juu.

GWIJI wa muziki wa Bongo Fleva ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi