loader
Dstv Habarileo  Mobile
City yadhamiria kumsajili Messi

City yadhamiria kumsajili Messi

KLABU ya Manchester City imedhamiria kuwaunganisha tena Lionel Messi na Pep Guardiola baada ya kumuogezea mkataba kocha huyo na kumfanya kuendelea na kazi hadi mwaka 2023.

Sasa City wataelekeza mawazo yao kumnasa Messi na kumuunganisha mchezaji huyo na kocha wake wazamani wa Barcelona, Guardiola wakati ndoto zao ni kutwaa kwa mara ya kwanza taji la Ligi ya Mabingwa wa Ulaya.

Messi,anatarajia kumaliza mkataba wake katika msimu ujao wa joto, yuko tayari kuondoka na City wanaweza  kumuondoa mapema mchezaji huyo hata Januari, ingawa inaonekana kumchukua kama mchezaji huru mwakani ni jambo linalowezekana.

Messi ambaye ni nyota wa kimataifa wa Argentina, awali alijaribu kuondoka Barca katika kipindi kilichopita cha majira ya joto, lakini aliamua kubaki ili kuepuka mgogoro wa kisheria dhidi ya klabu aliyoitumikia tangu utotoni, lakini sasa yuko tayari kuondoka mwishoni mwa msimu.

City imedhamiria kumnasa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 33 na inafikiri kumpata nyota huyo itakuwa karata yao muhimu katika mbio za kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa wa Ulaya.

Guardiola amejifunga kwa miaka miwili zaidi katika Man City na anataka kuipatia mataji zaidi likiwemo hilo la Ligi ya Mabingwa wa Ulaya, mashindano ambayo mara mbili alitwaa taji lake akiwa na Messi pale Barca, lakini ameshindwa kutwaa akiwa na Bayern Munich na

City.

Mkataba huo mpya wa Guardiola, una thamani ya Pauni milioni 20 kwa mwaka, ambao utamfanya kukaa Man City kwa miaka saba, na kuwemo katika orodha ya makocha waliokaa kwa muda mrefu katika klabu hiyo.

“Tangu niwasili Manchester City, wamenifanya nijisikie vizuri katika klabu na jiji hili kwa ujumla, “alisema Guardiola.

“Tangu wakati huo tumefanya mambo makubwa pamoja, kufunga magoli, kushinda mechi na mataji, na wote tunafurahia mafanikio kwa pamoja.

“Kupata ushirikiano ni jambo bora kwa kocha yeyote yule.

“Changamoto kwetu ni kendelea kuimarisha na kuwa bora zaidi na nimesisimka zaidi kuhusu kuisaidia Manchester City kufanya hivyo.”

Man City imetwaa mataji sita makubwa tangu waingie mkataba na kocha huyo wazamani wa Barcelona na Bayern Munich, mwenye umri wa miaka 49, mwaka 2016.

"Kulikuwa na ofa kutoka klabu za Juventus, Paris St-Germain na nyingine, lakini nina furaha zaidi kuendelea kuwepo hapa, “alisema kocha huyo Mhispania.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/720d10a22b3e1555a88c781d934001df.jpg

“Jesse Lingard atajifunza kutokana na makosa yaliyowapa faida ...

foto
Mwandishi: LONDON, England

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi