loader
Dstv Habarileo  Mobile
TPA
Picha

Wahitimu Mzumbe wapewa semina

Wahitimu wa kozi mbalimbali wa Chuo Kikuu Mzumbe wametakiwa kutovimba kichwa kwa elimu waliyopata, isipokuwa waitumie vyema elimu hiyo kushiriki na kuchangia katika kuujenga uchumi wa Tanzania.

 Hayo yalibainishwa jana na Mwenyekiti wa Baraza la Chuo cha Mzumbe Profesa Mathew Luhanga pamoja na Makamu Mkuu wa chuo hicho Profesa Lughano Kusiluka wakati wakizungumza kwa nyakati tofauti katika Mahafali ya 19 ya chuo hicho yaliyofanyika leo, Ijumaa (Novemba 20,2020) mkoani Morogoro.

"Tambueni sasa mnaenda kujiunga na Watanzania kulijenga Taifa, iungeni mkono serikali na kushiriki kikamilifu katika kuijenga nchi. Mnaaswa msivimbe kichwa hakikisheni popote mnapoenda msikiangushe chuo," alisema Profesa Kusiluka.

Alisema kuwa wahitimu hao wamepikwa na kuiva vizuri huku akiwaasa kufanya kazi kwa weledi na kutokiangusha chuo hicho

Profesa Kisukula amebainisha kuwa, mwaka huu pekee, chuo hicho kina jumla ya wahitimu wa kozi mbalimbali 3,751 lakini waliotunukiwa shahada zao leo ni 2,114.

Alieleza kuwa wahitimu 27 watatunukiwa katika kampasi ya chuo hicho iliyopo Mbeya mnamo Novemba 27, mwaka huu na wanne watatunukiwa katika kampasi ya Dar es Salaam Desemba 4, mwaka huu.

Akielezea mafanikio ya chuo hicho ndani ya miaka mitano chini ya Serikali ya Awamu ya Tano, Profesa Kusiluka alisema chuo kimetekeleza miradi mbalimbali yenye thamani ya Sh bilioni 15.

Aliitaja miradi hiyo kuwa ni ujenzi wa jengo la taaluma katika kampasi ya Mbeya lenye thamani ya Sh bilioni tatu, ujenzi wa hosteli za wanafunzi Sh bilioni 6.5 na ujenzi wa mradi wa ujenzi wa jengo la madarasa na kumbi za mihadhara Sh bilioni 3.1.

Aidha, alisema pia chuo hicho kimekarabati iliyokuwa Shule ya Jumuiya ya Wazazi Tegeta, Dar es Salaam ambayo sasa ni kampasi ya Mzumbe na itakuwa na uwezo wa kuchukua Wanafunzi 455.

Rais wa Tanzania Dk John Magufuli ...

foto
Mwandishi: Halima Mlacha

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi