loader
Dstv Habarileo  Mobile
Atletico kibaruani kwa Barcelona leo

Atletico kibaruani kwa Barcelona leo

TIMU pekee ambayo hadi sasa haijafungwa katika Ligi Kuu ya Hispania ya La Liga Atletico Madrid leo itakuwa katika mtihani mzito katika mbio zake za kuwania taji hilo wakati watakapokuwa wageni wa Barcelona.

Atletico katika msimamo wa La Liga wako katika nafasi ya tatu wakiwa na pointi 17 baada ya kushuka dimbani mara saba lakini wana mchezo mmoja mkononi wakati Barca wana pointi 11 katika nafasi ya nane wakijikusanyia jumla ya pointi 11.

Timu hiyo yenye maskani yake katika jiji la Madrid waliuanza msimu huu vizuri, wakishinda mechi tano na kutoka sare mara mbili katika mechi zao saba walizocheza hadi sasa wakiwa pointi tatu nyuma ya vinara Real Sociedad, huku wakiwa na michezo miwili mkononi.

Barcelona, wenyewe walianza vibaya chini ya kocha wao mpya, Ronald Koeman na baada ya kufungwa na Real Madrid na Getafe na vijana hao wa Catalans huenda wakateleza tena leo kama hawatakuwa makini.

Atletico huenda ikamkosa mchezaji wao Luis Suarez ambaye angeungana na timu yake yazamani baada ya kukutwa na Covid-19 wakati wa mechi za timu ya taifa wiki hii.

Mshambuliaji huyo wa Uruguay aliambiwa na Koeman kuwa anaweza kuondoka Camp Nou katika kipindi cha majira ya joto, lakini amedhihirisha umuhimu wake baada ya kufunga mabao matano katika mechi sita alizoichezea Atletico.

Tangu aanze kuifundisha Atletico mwaka 2011, Diego Simeone amewahi kuifunga Barca katika Ligi ya Mabingwa lakini hakuwahi kuwafunga katika mchezo wowote wa La Liga, na wengi wakitarajia leo itakuwa nafasi nzuri ya kubadili takwimu hizo.

Kikosi cha Simeone kinakwenda katika mchezo huo kikiwa hakijafungwa mechi zake 18 zilizopita za ligi kwenye uwanja wao wa nyumbani, ambapo mara ya mwisho walifungwa na Barcelona Desemba mwaka jana.

Lucas Torreira anaungana na Suarez katika orodha ya wachezaji wa Atletico, ambao hawatakuwepo, baada ya kukutwa na virusi vya corona, na Hector Herrera atakuwa nje kutokana na maumivu ya nyama za pata. Lakini taarifa njema ni kuwa mshambuliaji wao Diego Costa amerejea katika mazoezi wiki hii.

Barcelona wenyewe watamkosa Ansu Fati, ambaye kwa muda mrefu hayupo kutokana na maumivu ya goti, wakati Sergio Busquets naye pia hatakuwepo baada ya kujiumiza katika mechi ya taifa.

Kwingineko, baada ya kutolewa nishai na Valencia kwa kufungwa 4-1, Real Madrid watakuwa wenyeji wa timu iliyopo katika nafasi ya pili ya Villarreal katika mchezo utakaofanyika mapema leo Jumamosi.

Nahodha Sergio Ramos na pacha wake Raphael Varane wote waliumia wakati wa mechi za timu za taifa katikati ya wiki. Wawili hao wanaungana na washambuliaji Karim Benzema na Eden Hazard katika orodha ya wachezaji wanaoweza kukosa safari hiyo, wakati kiungo Federico Valverde anabaki kuwa nje baada ya kuvunjika mguu.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/afa5664ef9dc227e3bab74397f4b37ff.jpg

“Jesse Lingard atajifunza kutokana na makosa yaliyowapa faida ...

foto
Mwandishi: MADRID, Hispania

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi