loader
Dstv Habarileo  Mobile
TPA
Picha

‘Rais wa Tanga’ apigwa mvua 30 kwa mihadarati

MAHAKAMA Kuu, Kitengo cha Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, imemhukumu kifungo cha miaka 30 jela mfanyabiashara maarufu jijini Tanga, Yanga Omary maarufu kwa jina la ‘Rais wa Tanga’ kwa kusafirisha dawa za kulevya aina na heroine  zenye uzito wa gramu 1,052.63. 

 

Pia mahakama hiyo imewaachia huru washitakiwa wengine Rahma Juma, ambaye ni mke wa Yanga na Halima Mohamed, ambaye ni mfanyakazi wa ndani kwa kuwa ushahidi uliotolewa dhidi yao ulikuwa hafifu.

 

Hukumu hiyo ilisomwa na Jaji Imakulata Banzi katika Mahakama Kuu, Kanda ya Tanga. Alisema kuwa upande wa mashitaka ukiongozwa na Wakili wa Serikali Mkuu, Faraja Nchimbi, ulipitia ushahidi wa mashahidi saba na vielelezo 10  kuthibitisha pasipo kuacha shaka kuwa Yanga alikuwa akijihusisha na biashara hiyo haramu ya dawa za kulevya.

 

"Kwa kuzingatia ushahidi huo, mahakama hii inamtia hatiani mshitakiwa kwa kosa la kusafirisha dawa za kulevya kama alivyoshitakiwa," alisema Jaji Banzi.

 

Mawakili wengine waliokuwa wanawakilisha jamhuri katika shauri hilo ni Wakili Mwandamizi, Pius Hilla, Mawakili wa Serikali , Constantine Kakula, Salimu Msemo, Donata Kazungu na Mseley Mfinanga, ambaye ni mwanasheria mwandamizi kutoka Mamlaka ya Kuzuia Dawa za Kulevya (DCEA).

Akieleza kuhusu kuachiwa washtakiwa namba mbili na namba tatu Jaji Banzi alisema kuwa upande wa mashitaka umeshindwa kuthibitisha shitaka hilo dhidi yao kwa kuwa tangu awali taarifa za mashitaka zilikuwa zikimhusisha mshitakiwa wa kwanza, Yanga .

Alieleza kuwa Rahma ambaye ni mke wa Yanga hakuhusishwa kwa namna yoyote na mashitaka hayo tangu mwanzo na kwamba mshitakiwa wa tatu alikuwa mfanyakazi wa ndani , lakini mbali na hivyo vitu vilivyokutwa chumbani kwake vilithibitika kuwa si dawa za kulevya.

Katika shauri hilo washtakiwa hao walikuwa wakiwakilishwa na Mawakili wa utetezi Majura Magafu, Nehemia Nkoko, Mohamed Kajembe, Kahoza Nicholaus na Denis Tumaini.

Rais wa Tanzania Dk John Magufuli ...

foto
Mwandishi: Anna Mwikola

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi