loader
Dstv Habarileo  Mobile
TPA
Picha

Simba, Azam kazi wanayo

LIGI Kuu Tanzania Bara raundi ya 11 inatarajiwa kuendelea leo kwa michezo minne kuchezwa, huku mabingwa watetezi Simba watakuwa ugenini  kusaka pointi tatu muhimu dhidi ya Coastal Union kwenye Uwanja wa Sheikh amri Abeid Jijini Arusha.

Simba wanashika nafasi ya tatu baada ya kucheza mechi 10 wanaingia kwenye mchezo huo wa 11 wakiwa na pointi 20 wakipania kusaka pointi tatu muhimu ili kuwasogelea Azam na Yanga zilizopo katika nafasi ya kwanza na pili.

Pia timu hiyo inatarajiwa kuongezewa nguvu baada ya kurejea kwa nyota wake, Bernard Morrison aliyefungiwa mechi tatu baada ya kumpiga ngumi Juma Nyoso, Simba walipocheza dhidi ya Ruvu Shooting na kufungwa 1-0.

Wanakutana na Coastal Union waliopo katika nafasi ya 11 kwenye msimamo wa ligi hiyo wakicheza michezo sawa na Simba, wakipoteza michezo minne na sare tatu inayochangiwa na kukosa muunganiko wa kikosi chao ni moja ya sababu iliyowafanya kukusanya pointi 12.

Coastal wanachezea Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha baada ya uwanja wao wa Mkwakwani jijini Tanga kufungia kutokana na kutokidhi haja.

Katika mchezo mwingine leo, Azam wanaoongoza ligi hiyo wakiwa na pointi 25 watakuwa ugenini kuwakabili KMC FC mchezo utakaofanyika kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Ni miongoni mwa michezo unaotarajiwa kuwa na ushindani mkali kwani timu zote tangu ianze ligi zimekuwa zikionesha kandanda safi, licha ya KMC kushikilia nafasi ya saba  wakiwa na jumla ya pointi 15.

Mechi zingine Polisi Tanzania itakwaana na dhidi ya Ihefu kwenye Uwanja wa Chuo cha Ushirika mjini Moshi wakati JKT Tanzania watapepetana na Gwambina FC kwenye Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.

Wakati huohuo, timu ya Ruvu Shooting imeng’ara jana katika mchezo wake wa  Ligi Kuu baada ya kuichapa Mbeya City mabao 3-0, uliochezwa kwenye Uwaja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Mabao yalifungwa na William Patrick dakika ya 12, Abrahaman Mussa dakika 53 na Fullyzulu Maganga akimalizia bao la tatu dakika ya 90 kwa kichwa. 

Mchezo mwingine ulikuwa katika uwanja wa Jamhuri Dodoma wenyeji Dodoma jiji wakilazimishwa sare ya bao 1-1 huku Tanzania Prisons wakitoka suluhu dhidi ya Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Nelson Mandela, Sumbawanga.

KOCHA wa Yanga, Cedric Kaze amewashusha ...

foto
Mwandishi: Waandishi Wetu

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi