loader
Dstv Habarileo  Mobile
TPA
Picha

Dk Mwinyi atoa maagizo mawaziri wapya

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Hussein Mwinyi leo amewaapisha mawaziri 15 ambapo amewataka kuwa na hati nne kwa ajili ya kutengeneza mpango kazi kwa ajili ya wizara zao katika kipindi cha miaka mitano ikiwemo kufahamu vizuri muundo wa wizara na taasisi zote zilizopo chini yake.

Akizungumza katika hotuba yake Ikulu Zanzibar, Dk Mwinyi aliwashukuru mawaziri wote kwa kukubali uteuzi huo na kubainisha kuwa hakuna aliyemtaarifu juu ya uteuzi wake.

Hati ambazo mawaziri hao wanatakiwa kuwa nazo ili kutengeneza mpango kazi katika wizara zao kwa kipindi cha miaka mitano ni kama ifuatavyo;

1.Ilani ya uchaguzi inasema nini katika wizara 

2.Hotuba aliyotoa katika Baraza la Wawakilishi inaelekeza nini kwenye wizara 

3.Ahadi  kipindi cha kampeni zinasemaje

4.Kupata maoni ya wadau kuhusu wizara    

Katika hatua nyingine Dk Mwinyi amewataka mawaziri waliokula kiapo kuwajibika ipasavyo na kuhakikisha kila mtumishi anatekeleza wajibu wake kwa wananchi.

     

Rais wa Tanzania Dk John Magufuli ...

foto
Mwandishi: Alfred Lukonge

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi