loader
Dstv Habarileo  Mobile
TPA
Picha

DC aagiza upembuzi mabonde ya umwagiliaji

Mkuu wa Wilaya ya Songea, Pololeti Mjema ametaka mabonde matatu yaliyopo katika Kijiji cha Nakahuga, Peramiho  wilayani  Songea, mkoani Ruvuma yafanyiwe pembuzi yakinifu ili yaweze kutumika katika kilimo cha umwagiliaji.

Alitoa agizo hilo wakati akizungumza na wataalamu kutoka Tume ya Taifa ya umwagiali waliopo mkoani humo katika ziara ya kuelemisha wakulima, katika skimu za kilimo cha umwagiliaji za Nakahunga wilayani Songea, HangaNgadinda wilayani Madaba, na kimbande na Msanjesi wilayani Nyasa.

Lengo la kuwa na  skimu hizo ni kupanua eneo la kilimo cha umwagiliaji kutoka hekta zaidi ya laki sita  zinazomwagiliwa kwa sasa nchini, kufikia hekta milioni moja na laki mbili ifikapo mwaka 2025.

Mjema, alisema kuwa, Serikali kupitia wizara ya kilimo, ilishatoa fedha  kupitia halmashauri husika ili uendelezaji ufanyike.

Aliwataka wataalamu hao kuwaelekeza wakulima nia ya serikali na hivyo kuwa tayari kuchangia katika mfuko wa maendeleo ya kilimo cha umwagiliaji ili kuwe na utunzaji na uboreshaji thabiti wa miundombinu hiyo.

Alkiwataka pia wataalamu kwenda kusisitiza suala zima la utunzaji wa mazingira na matumizi ya raslimali maji ili wakulima waweze kunufaika.

Akizungumza wakati wa kutoa elimu kwa wakulima katika skimu ya Nakahuga iliyopo Peramiho, Mkurugenzi msaidizi wa Idara ya uendeshaji na matunzo kutoka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji, Enterbert Nyoni, alisema mafunzo hayo yatawasaidia wakulima kuelewa sheria ya Taifa ya umwagiliaji ya mwaka 2013 na namna ya kuchangia tozo za huduma za umwagiliaji.

Rais wa Tanzania Dk John Magufuli ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Maalumu, Songea

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi