loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Watafiti watakiwa kutatua changamoto za jamii

MKUU wa Mkoa wa Dodoma, Dk Binilith Mahenge amewataka watafiti kufanya kazi zao vyema kwa lengo la  kutatua changamoto zinazojitokeza katika jamii .

Alisema hayo wakati akizungumza katika kongamano la kitaaluma lilioandaliwa na Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE),

Alisema wakati umefika kwa watafiti watanzania kujikita katika kutatua matatizo ya watanzania badala ya kutegemea watafiti wa nje ambao wanafanya kwa makusudio yao binafsi.

"Wakati mwingine najua huwa tunapata wasimamizi kutoka nje ya nchi ambaye kwenye kuchagua hiyo research topic (mada ya utafiti) yako anaweza kuwa na mwonekano wa upendeleo wa upande wake,"alisema.

Aidha katika hotuba yake aliwapongeza CBE kwa kufanya utafiti katika eneo la wafanyabiashara ndogo ndogo maarufu kama machinga ambao unalenga kutatua changamoto walizonazo.

Naye mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Ali Gugu alisema machapisho yanayotolewa na chuo hicho yanalenga katika kuisaidia jamii na Taifa kwa ujumla.

Awali, Mkuu wa Chuo Cha CBE, Profesa Emanuel Mjema alisema chuo kimeendelea kutoa mafunzo, kufanya tafiti na kutoa ushauri katika sekta ya viwanda na biashara.

Alisema moja ya  changamoto ya juu iliyoibuliwa na tafiti hizo ni ya  kurasimisha shughuli za wafanyabiashara ndogo ndogo ili kukuza mitaji yao pamoja na kuchangia pato la Taifa kupitia ulipaji wa kodi.

"Machinga tunafikiri ni biashara ndogo lakini kumbe ni biashara kubwa na inahusisha watu wengi sana kwa hiyo inatoa ajira nyingi sana kwa hiyo tukiirasimisha inaweza kuchangia kodi katika nchi yetu,"alisema.

WAZIRI wa Maji, Jumaa Aweso amesema serikali imeweza ...

foto
Mwandishi: Anastazia Anyimike, Dodoma

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi