loader
Dstv Habarileo  Mobile
TPA
Picha

Vifaa tiba vyawasili  kituo cha afya Kitunda

VIFAA tiba vyenye thamani ya zaidi ya Sh milioni 8.3 vimefikishwa katika Kituo cha Afya Kitunda na zahanati ya Kamata namba 3 wilayani Sikonge mkoani Tabora.

Vifaa hivyo vimetolewa na Kampuni PowerCorner (T)  ikiwa ni kuunga mkono juhudi zinazofanywa na serikali ya awamu ya 5 ya Rais John Magufuli katika kuboresha huduma za afya na miundombinu ya zahanati, vituo vya afya na hospitali mbalimbali hapa nchini.

Kufikishwa kwa vifaa hivyo kutawezesha wananchi wa vijiji vya Mgambo, Mwenge na Mkola vilivyoko katika kata ya Kitunda wilayani Sikonge kunufaika na huduma za afya na kupunguza safari za kwenda Sikonge kufuata huduma.

Akizungumza  jana Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya hiyo Tito Luchagula alisema kuwa vifaa hivyo vimekuja wakati mwafaka kutokana na kero kubwa waliyokuwa wakipata wakazi wa vijiji hivyo na maeneo jirani wanapougua na kuja kupata huduma katika Kituo hicho na zahanati.

Alibainisha kuwa vifaa hivyo vitaboresha kwa kiasi kikubwa huduma za afya kwa mama na mtoto na wagojwa wa nje wanaohitajika kulazwa .

Mganga Mkuu wa wilaya hiyo Dk Theopista Elisa alibainisha baadhi ya changamoto zilizowakabili kituo hicho kuwa ni pamoja uhaba wa vifaa tiba, uchakavu wa gari la wagonjwa na upungufu wa watumishi.

Aidha alisema kutokamilika jengo la kufulia na ukosefu wa wodi ya kusubirisha wajawazito  nui kero nyingine iliyobaki na kuwaomba wadau wengine kusaidia.

Awali akikabidhi vifaa hivyo Meneja wa PowerCorner (T) Ltd Kanda ya Magharibi Erick Frank alisema kuwa wametoa vifaa hivyo baada ya kuombwa na uongozi wa Kituo cha afya Kitunda na zahanati ya Kamata namba 3 kutokana na changamoto wanazopata wananchi.

Alitaja vifaa vilivyotolewa kwa ajili ya Kituo cha afya kuwa ni vitanda 12 vya wagonjwa, magodoro12, mito 24, meza 1, mabenchi 10, viti 2 na vifaa vya kunawia mikono 3 vyote vikiwa na thamani ya sh 6,489,000.

Na katika zahanati ya Kamata namba 3 inayohudumia wakazi wa kijiji cha Mwenge/Mkola walitoa vitanda vya wagonjwa 3, magodoro 3, meza 2, viti 4, mito 6 na dawa ya kunawia mikono vyenye thamani ya sh 1,886,000/-.

Meneja Biashara wa Kampuni hiyo Vyuvian Katala alisema kuwa Power Corner (T) Ltd itaendelea kutoa msaada katika kituo hicho na maeneo mengine ili kuunga mkono juhudi za serikali katika utoaji huduma za afya kwa jamii.

Alibainisha kuwa msaada huo ni sehemu ya mchango wa kampuni hiyo inayojihusisha na uzalishaji na usambazaji umeme utokanao na nguvu ya jua kwa jamii iishio vijijini kili uhakikisha huduma za afya zinaendelea kuboreshwa katika eneo lenye mradi wao.

Rais wa Tanzania Dk John Magufuli ...

foto
Mwandishi: Na Lucas Raphael, Sikonge

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi