loader
Dstv Habarileo  Mobile
TPA
Picha

Kasi ya kufyeka misitu ya asili yatisha

INAKADiRIWA hekta milioni 7.3 za misitu hupotea kila mwaka duniani na kwamba Afrika kwa kupoteza hekta milioni 3.94 kati ya mwaka 2010 na 2020.

Hayo yaliezwa jana mkoani hapa na mratibu wa mradi wa uhifadhi misitu ya miombo, ofisi ya shirika la chakula na kilimo duniani (FAO) nchini Tanzania, Geofrey Bakanga.

Akitoa taarifa kwa niaba ya mwakilishi mkazi wa Shirika la Chakula na Kilimo Duniani (FAO) Ofisi ya  Tanzania alisema misitu ni suala ambalo liko wazi kwa kila mtu na kwamba  maisha ya kila mtu yanategemea misitu.

Bakanga  alisema chanzo  kikuu cha uharibifu ni pamoja na kuongezeka kwa idadi ya watu,shughuli za kijamii na kiuchumi ikiwemo upanuzi wa mashamba kwa shughuli za kilimo,ufugaji wa mifugo mingi katika maeneo madogo.

Hata hivyo alisema kuwa ili kutatua tatizo la changamoto hiyo inahitajika njia jumuishi ili waunganishe mipango yao kwa kila sekta ambapo alisema kuwa mfuko wa dunia wa kuhifadhi mazingira (GEF)katika awamu yake ya 7 ya mgawanyo wa fedha katika kusimamia mazingira umelenga kusaidia nchi zinzoendelea kutatua tatizo hilo kwa kuja na mpango maalumu wa kuonyesha matokeo.

Kwa upande wake Kamishina msaidizi wa uhifadhi Dk Hamza Katey akisoma hotuba kwa niaba ya Kamishina wa uhifadhi misitu, Wakala wa Huduma  za Misitu Tanzania Prof Dos Santos Silayo alisema kuwa Serikali kupitia wakala wa huduma ya misitu Tanzania TFS kwa kushirikiana na shirika FAO inaendelea kutekeleza mradi wa kuzuia uvunaji holela wa miti.

Katey alisema kuwa mradi huo unalenga kung’oa na kuzuia uharibifu wa ardhi na upotevu wa bionuai katika ikolojia ya misitu ya miombo ya nyanda kame.

Naye Ofisa Mazingira Mwandamizi kutoka katika Ofisi ya Makamu wa Rais Thomas Chali alisema kuwa  lengo la mkutano huo ni uhakiki wa mradi na kwamba kikao hicho ni muhimu kwa nchi hivyo aliwataka kutambua  kuwa wanajukumu kubwa la kuhakikkisha wanaitendea haki nchi.

Rais wa Tanzania Dk John Magufuli ...

foto
Mwandishi: Agnes Haule,Morogoro

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi