loader
Dstv Habarileo  Mobile
TPA
Picha

Soko la Loliondo lapunguza tozo kwa wadau

UONGOZI wa soko la Loliondo wilayani Kibaha umewapunguzia gharama mbalimbali ikiwemo ya ulinzi na maji  wadau wake.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi ofisini kwake mwenyekiti wa soko hilo Mohamed Mnembwe alisema kuwa gharama zilikuwa kubwa na wafanyabiashara wengi walikuwa wakilalamika.

Mnembwe alisema kuwa uongozi wao ambao umeingia mwaka huu ulikuwa ukiombwa kupunguza gharama mbalimbali ikiwa ni pamoja na ulinzi .

Alisema wamekubali ombi la wafanyabiashara kwamba kutoka shilingi 150,000 sasa watakuwa wakilipa 100,000 kwa wale wanaouza matunda.

"Wafanyabiashara wanaouza bidhaa mchanganyiko walikuwa wakilipa kiasi cha shilingi 300,000 kwa ajili ya ulinzi sasa watalipa 200,000 ambapo wale wa mchele walikuwa wanalipa 400,000 sasa watalipa 300,000,"alisema Mnembwe.

Alisema kuwa wafanyabiashara wa nyanya walikuwa wanalipia ulinzi 20,000 lakini kwa sasa watalipa 2,000 na wale wanaouza vitu kama nyanya, viazi na ndizi mbichi wanalipa 100,000.

Alisema kuwa mkakati walionao ni kuanzisha chama cha kuweka na kukopa Saccos badala ya wafanyabiashara kwenda kukopa kwenye taasisi za kifedha ambazo zimekuwa zikiwatoza riba kubwa na kusababisha biashara kushindwa kukuwa.

Aidha alisema kuwa kwa sasa wanaendelea na majadiliano na vikao navyo vinaendelea lakini mkutano mkuu maalumu kwa ajili hiyo utafanyika Januari mwakani kwa ajili ya kulipitisha hilo ambapo soko hilo lililohamishwa kutoka ilipokuwa stendi ya zamani lina wafanyabiashara 800.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es ...

foto
Mwandishi: John Gagarini, Kibaha

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi