loader
Dstv Habarileo  Mobile
TPA
Picha

Watuhumu uongozi wa kijiji kuuza ekari 1,200 za ardhi

WANANCHI wa Kijiji cha Ibutamisuzi kata ya Mbutu wilayani Igunga mkoani Tabora wamewatuhumu viongozi wao wa serikali ya Kijiji kwa kuuza eneo la Kijiji chao.

Wamedai kuwa zaidi ya ekari 1,200 zimeuzwa kwa mfugaji na kula  Sh milioni 5 za Kijiji hicho.

Viongozi wanaotuhumiwa kuuza eneo hilo ni pamoja na mwenyekiti wa serikali ya Kijiji hicho Benedictor Golani Mangwiwa na mtendaji wa Kijiji hicho Ludovick Ngassa.

Wakizungumza na waandishi wa habari Kijiji hapo baadhi ya wananchi hao Kizanga Luhende, Mwashi Kulindwa, Hadija Jelemia, na Lazaro Jackson walisema viongozi wao waliuza eneo hilo kwa mfugaji Masheni Mboje.

Aidha Jeremia aliongeza kuwa pamoja na viongozi hao kuuza eneo la Kijiji pia wamekula fedha Sh milioni 5 ambapo fedha hizo zililipwa na mkulima waliyemtaja jina moja la Kagi aliyekodi ekari 1000 za eneo la Kijiji ili alime zao la pamba .

Kwa upande wao viongozi hao wa serikali ya Kijiji hicho cha Ibutamisuzi mtendaji Kijiji Ludovick Ngassa na mwenyekiti wake wa Kijiji Benedictor Mang'wiwa walipoulizwa juu ya tuhuma hizo walikanusha kuuza eneo hilo wala kula fedha.

Naye mfugaji huyo Masheni Mboje alikiri kumiliki ekari hizo alizosema alipewa na serikali ya Kijiji na mwenye shida ya eneo hilo aende mahakamani.

Kwa upande wake Diwani wa kata hiyo ya Mbutu CCM Lucas Bugota alithibitisha kutambua tuhuma hizo na kusema kuwa serikali ya Kijiji hicho imeshindwa kufuatilia suala hilo.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es ...

foto
Mwandishi: Na Mwandishi Wetu , Tabora

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi