loader
Dstv Habarileo  Mobile
TPA
Picha

Ndugai aahidi Bunge la 12 kulinda haki za watoto

SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai amesema Bunge la 12 litahakikisha linashughulikia agenda za watoto na vijana ili kusaidia Serikali kufikia malengo endelevu ya dunia.

Ndugai, aliyasema hayo jana wakati akitoa hotuba yake kwenye maadhimisho ya siku ya mtoto Duniani yaliyofanyika katika ukumbi wa Msekwa Bungeni jijini Dodoma.

Alisema, wabunge wanatakiwa kusoma kitabu cha ajenda za watoto na vijana kilichotolewa na Shirika la Kuhudumia Watoto Duniani (Unicef), ili kuzielewa na kuisaidia serikali kutekeleza masuala mbalimbali ambayo imesaini katika mikataba ya kimataifa.

"Bunge letu tukufu tayari lilishaingia makubaliano yaani MOU, na shirika linalojihusisha na masuala ya watoto duniani (Unicef) katika kusaidia kupambania haki za watoto,"alisema Ndugai.

Alisema bunge lake lipo tayari kufanya kazi na mashirika mbalimbali nchini na yale ya kimataifa  kusaidia kulinda haki za watoto na vijana.

 

Alitoa mwito kwa Unicef kutoa elimu kwa wabunge kwa njia ya semina, mafunzo pamoja ziara ya kutembelea maeneo mbalimbali ili kujifunza mambo yanayohusu haki ya mtoto.

Mratibu mkazi wa Shirika la UN, Zlatan Milisic alipongeza serikali  kwa jitihada inazozifanya  kulinda haki za mtoto.

Kwa mujibu Milisic, maadhimisho ya siku ya mtoto duniani mwaka huu yanafanyika ikiwa imepita miaka 31 kutoka mkataba wa kimataifa kuhusu kulinda haki za mtoto usainiwe.

Awali, mtoto kutoka Mbeya Agape Joster (13), aliwaeleza wabunge kuwa wanakabiliwa na changamoto  mbalimbali hasa ukosefu wa mabweni kwa wanafunzi wa shule za kata hali inayosababisha wengi wao kupata mimba.

 

Mkuu wa Wilaya, Gift Msuya kwa niaba ya Mkuu ...

foto
Mwandishi: Anastazia Anyimike, Dodoma

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi