loader
Dstv Habarileo  Mobile
TPA
Picha

Saccos ya Hazina kununua mikopo ya wanachama wake

CHAMA Cha Ushirika wa Akiba na Mikopo cha Hazina kimepanga kununua mikopo  ya wanachama wake  waliyoipata  kutokana na fedha za Bodi ya Mikopo kwa wanafunzi wa  elimu ya juu.

Hatua hiyo itasaidia wanafunzi wengi zaidi wanaodaiwa na Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB)  lakini pia ikiwaacha huru wanachama hao na kuendelea kulipa katika chama hicho.

Aidha kina mpango wa kushusha riba ya mikopo kwa chama hicho kutoka asilimia mbili hadi asilimia 1.5 jambo litakalosaidia kuwapo kwa uendelevu kwa chama hicho na wengi kunufaika.

Mwenyekiti wa  Hazina Saccos,Aliko Mwaiteleke alisema hayo jana jijini Dar es Salaam katika mkutano mkuu wa saba wa chama hicho, ambao pia wanachama wake watafanya uchaguzi kwa viongozi na bodi ya chama.

Kuhusu kununua mikopo alisema wanachama wengi wa Hazina Saccos wamekuwa wakiomba mikopo wanayodaiwa na HESLB  iweze kununuliwa na chama hicho, badala ya kuendelea kuwajibika kwa chama na kwa bodi pindi wanapokuwa na mikopo.

"Kwa muhtasari huo, wanachama hao wanaomba kile wanachodaiwa na Bodi ya Mikopo kinunuliwe na Chama cha  Hazina ili wao waendelee kulipa kwa Hazina moja kwa moja," alisema Mwaiteleka na kuongeza kuwa chama hicho kina wanachama zaidi ya 4,000 na mtaji wa sh bilioni 12.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Mkurugenzi Msaidizi, Rasilimali Watu, Gisela Mugumira alisema serikali inawataka watumishi wa serikali ambao ndio wanachama wa Hazina kutambua kuwa wamebeba dhana ya maendeleo na kwamba chama hicho kiendelezwe na kuwafikia watumishi walio wengi.

 

 

MAFUNDI umeme nchini wametakiwa kufanya ...

foto
Mwandishi: Lucy Lyatuu

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi