loader
Dstv Habarileo  Mobile
TPA
Picha

Mamlaka za kisheria maeneo ya madini yafanunuliwa

KATIBU Mkuu, Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila amesema migogoro ya wachimbaji wa madini inayohusu masuala ya madini haiwezi kutatuliwa kwa matamko ya Baraza la Ardhi kwa kuwa kila sheria inatumika mahala pake.

Amesema migogoro ya namna hiyo hutatuliwa kwa kuzingatia kwanza matakwa ya Sheria ya Madini.

Alisema hayo jana alipotembelea eneo la  mgogoro wa wachimbaji wadogo kati ya vikundi vya wachimbaji wadogo wa Mwime na Isalenge katika mkoa Shinyanga Wilayani Kahama.

Mgogoro huo kati ya vikundi hivyo, uliibuka baada ya vikundi  viwili kutofautiana wakati wakigombea  kuteuliwa na Tume ya Madini kusimamia eneo la mlipuko wa madini ya dhahau  la Mwime wilayani Kahama.

Katika mchakato wa kumpata atakayepewa jukumu hilo la usimamizi, kamati iliyoteuwa na Mkuu wa Wilaya ya Kahama Anamringa Macha ilikipa ushindi kikundi cha Isalenge baada ya kukidhi vigezo vilivyowekwa.

Kamati hiyo ilikuwa na makundi mbalimbali kutoka katika ofisi ya wilaya na Ofisi ya Tume ya Madini ya wilaya.

Kutokana na uamuzi huo, kikundi cha Mwime hakikuridhia kikundi cha Isalenge kupewa kazi hiyo ndipo walikwenda kushitaki kwenye Baraza la Ardhi la Wilaya nalo likatoa tamko la kutengua uamuzi wa Kamati ya Mkuu wa Wilaya kwa kufuata matakwa ya Sheria ya Ardhi.

“Kamati hii haikuwa na upendeleo. Hoja iliyotumika kukipa ushindi kikundi cha Iselange ni kutoka na kukidhi vigezo vilivyopangwa” alisema Macha.

Baada ya Baraza la Ardhi kutengua uamuzi wa kamati ya Mkuu wa Wilaya, Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini alisema maamuzi ya Baraza la Ardhi hayawezi kutatua mgogoro huo kwa sababu sheria za Ardhi haziingiliani na Sheria za Madini na kwamba maagizo hayo hayawezi kutekelezwa.

“Baraza la Ardhi halina mamlaka ya kutatua mgogoro wa wachimbaji wadogo unaohusu masuala ya kimadini. Agizo la Baraza la Ardhi ni batili na halitekelezeki,” alisema Profesa Msanjila.

MAFUNDI umeme nchini wametakiwa kufanya ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Maalumu

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi