loader
Dstv Habarileo  Mobile
Guardiola: Nataka Messi amalize soka Barcelona

Guardiola: Nataka Messi amalize soka Barcelona

KOCHA Pep Guardiola, aliyesaini nyongeza ya mkataba wa miaka miwili na klabu ya Manchester City, Alhamisi iliyopita anahusishwa na mchezaji wake wa zamani, Lionell Messi kukaribia kuhamia klabu hiyo msimu uliopita wa majira ya joto.

Mkataba wa Messi unamalizika msimu ujao wa kiangazi na anaweza kusaini makubaliano ya awali ya mkataba na klabu yoyote nje ya Hispania kuanzia Januari Mosi.

Guardiola alisema: "Messi ni mchezaji wa Barcelona. Nilisema mara elfu moja. Kama shabiki, nataka amalizie soka hapo."

Mchezaji  huyo wa timu ya Taifa ya Argentina Messi ameonekana kutaka kujiunga na City baada ya kuweka ombi la uhamisho Agosti mwaka huu, kwa rais wa wakati huo wa Barcelona, Josep Maria Bartomeu kuzuia uhamisho huo.

Bartomeu alijiuzulu Oktoba lakini hatima ya Messi bado haijulikani.

"Mkataba wake unamalizika mwaka huu [msimu] na sijui ni nini kitatokea akilini mwake," Guardiola alisema.

Paris St-Germain pia imekuwa ikihusishwa na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 33, lakini kila mgombea katika uchaguzi wa urais wa Barcelona utakaofanyika Januari mwakani amesema ni kipaumbele kwao ni kumshawishi Messi abaki.

"Nina shukrani kubwa kwa Barcelona na kile walichonifanyia," alisema Guardiola, ambaye alifanya kazi na Messi wakati akisimamia klabu hiyo kati ya 2008 na 2012.

"Katika akademi, kama mchezaji na kocha , walinipa kila kitu kabisa. Hivi sasa Messi ni mchezaji wa Barcelona na soko la uhamisho liko Juni na Julai.

"Tunayo michezo mzuri na malengo na vitu ambavyo tungependa kufanikiwa. Hilo ndilo jambo pekee katika akili zetu. Mengine, siwezi kusema chochote."

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/1d776219260b546134d0050095ac45d6.jpg

“Jesse Lingard atajifunza kutokana na makosa yaliyowapa faida ...

foto
Mwandishi: LONDON, England

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi