loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Chuo cha uandishi cha MSJ, OUT kushirikiana

IDARA ya Uandishi na Masomo ya Habari (DJMS) ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT) na Chuo cha Uandishi wa Habari cha Morogoro (MSJ) watashirikiana katika utoaji wa elimu ya fani za uandishi wa habari na mawasiliano ya umma ili kuandaa wahitimu bora zaidi watakaokidhi vigezo vya soko la ajira.

Hayo yalibainika wakati wa mkutano wa kwanza kati ya Idara ya Uandishi na Masomo ya Habari (DJMS) ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania na uongozi wa Chuo cha Uandishi wa Habari cha Morogoro yaliyofanyika mjini Morogoro jana na kuhudhuriwa na wawakilishi wa pande zote mbili.

Mkurugenzi wa Kituo cha OUT Mkoa wa Morogoro, Dk Wambuka Rangi alisema OUT itashirikiana na MSJ katika ufundishaji wa nadharia na mafunzo kwa vitendo kwa wanafunzi wa fani za habari na mawasiliano ya umma kwa kutumia rasilimali watu, vifaa na kiufundi zilizopo katika taasisi hizo.

“OUT kama ilivyo vyuo vingine duniani kinafanya utafiti, ushauri wa kitaalamu na ufundishaji na kimedhamiria kuwafikia watu wote mahali walipo katika utoaji wa elimu bora na kwa gharama nafuu,”alisema.

Alisema elimu huria na masafa inahitaji mtu mwenye uelewa wa masuala ya Teknolojia ya Habari na Mawasilano (Tehama), kitu ambacho mtu anaweza kujifunza kwa muda mfupi na akaendelea na masomo katika fani ya uchaguzi wake.

Mkuu wa MSJ, Marko Kanga alisema lengo la makubaliano hayo yanalenga namna bora ya kutumia rasilimali zilizopo kwa pande zote mbili ili kurahisisha utoaji wa elimu katika tasnia ya habari.

WAZIRI wa Nishati na Madini, Dk ...

foto
Mwandishi: Vincent Mpepo, OUT

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi