loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Maofisa kilimo, wakulima wa korosho Moshi wapewa neno

MAOFISA kilimo na wakulima wa zao la korosho wilayani Moshi mkoani Kilimanjaro wametakiwa kusambaza vizuri na kwa kasi kubwa elimu inayotolewa na wataalamu wa zao hilo kuhusu kupanda mbegu bora za korosho ili kuleta mafanikio chanya ya kilimo hicho wilayani humo.  

Kauli hiyo ilitolewa hivi karibuni na Mrakibu Mwandamizi wa Gereza kuu Karanga, Frank Mwakijungu wilayani Moshi mkoani Kilimanjaro wakati wa mafunzo ya siku mbili kwa wakulima wa zao la korosho.

Mafunzo hayo ni kuhusu kilimo bora cha zao la korosho na ubora wake yanayoendeshwa na Bodi ya korosho Tanzania(CBT) kwa kushirikiana na TARI Naliendele, lengo likiwa kuwapatia wakulima hao teknolojia mpya za kilimo bora cha zao la korosho kwa kupanda mbegu bora na kudhibiti wadudu waharibifu na magonjwa katika zao hilo.

 

Alisema wenye jukumu la kuifanya elimu hiyo kuweza kusambaza kwa kasi au kuwafikia kikamilifu wakulima na wadau wengine na korosho ni maofisa kilimo pamoja na wakulima ambao wameshiriki mafunzo wilayani humo.

Kwa upande wake mtaalamu kutoka TARI Naliendele, Dadili Majune alisema wakulima wilayani humo baada ya kupokea mbegu nyingi kutoka Tari Naliendele wamehamasika kupanda  mikorosho lakini walikuwa na tatizo la namna ya kudhibiti wadudu waharibifu ambao ni mbu wa mikorosho na mbu wa minazi pamoja na magonjwa na baada ya kuletewa elimu hiyo wamefurahishwa kwani itawasaidia na kuongeza tija kwenye zao la korosho.

WAZIRI wa Nishati na Madini, Dk ...

foto
Mwandishi: Sijawa Omary, Moshi

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi