loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

NICOL yaahidi makubwa kwa wanahisa wake

KAMPUNI ya uwekezaji ya NICOL imeahidi kuendelea kuongeza gawio kwa wanahisa wake kutokana na mipango mizuri ambayo imewekwa na uongozi ya kuwekeza kwenye miradi yenye faida.

Hayo yalisemwa mwishoni mwa wiki na Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni hiyo, Dk Gideon Kaunda, wakati wa Mkutano Mkuu wa mwaka wa kampuni hiyo uliofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.

Alisema uongozi mpya wa kampuni hiyo umefanya kazi kubwa mpaka kuongeza gawio kutoka Sh sita zilizotolewa mwaka jana kwa wanahisa wake mpaka kufikia Sh 10 iliyotolewa  mwaka huu.

Alisema anaamini mambo yataendelea kuwa mazuri kwani wamewekeza kwenye kampuni kubwa kama Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Benki ya NMB, Soko la Hisa Dar es Salaam (DSE), Kampuni ya Simu ya Vodacom na kwenye viwanda vya uzalishaji wa saruji.

Alisema uongozi wa sasa wa NICOL unapata ushirikiano mkubwa kutoka vyombo kama Mamlaka ya Masoko na Mitaji (CMCA) na DSE ambao wamekuwa wakiwapa miongozo na maelekezo ya namna ya kutatua changamoto wanazokumbana nazo.

Alisema kuna wawekezaji kutoka nje ya nchi kama Marekani na Australia, hivyo aliwahimiza watanzania wengi zaidi kuiunga mkono kampuni hiyo kwani inakwenda vizuri na watanufaika na uwekezaji wao.

“Wanahisa wa NICOL wana imani kubwa na menejimenti yao na wamekuwa wakitoa ushirikiano mkubwa na kwenye kura ya mapendekezo tuliyoyatoa wengi walikuwa wakiyakubali ndiyo maana yote yamepita kwa zaidi ya asilimia 90,”alisema.

Alisema tangu waingie madarakani mwaka 2012 wamekuwa wakitoa gawio kwa wanahisa wao hata pale wanapopata changamoto wamekuwa wakitoa tofauti na ilivyokuwa kabla hawajaichukua.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Fedha wa NICOL, Erasto Ngamilaga alisema kuna dalili njema za kukua kwa kampuni hiyo na kuendelea kutoa gawio zuri kwa wanahisa wake.

“Tutaendelea kuongeza kwa namna tunavyopata mafanikio kwenye uwekezaji nawaambia wanahisa NICOL wajivunie kuwa kwenye kampuni yenye mwelekeo sahihi nawaomba ambao hawajanunua hisa waje kununua,”alisema.

NAIBU Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi