loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

DSE yazindua mfumo wa kununua ‘Hisa Kiganjani’

 

SOKO la Hisa la Dar es Salaam (DSE) limezindua mfumo wa kuuza na kununua hisa kwa njia ya simu za mkononi ujulikanao kama ‘Hisa Kiganjani’ ambao pamoja na mambo mengine umelenga kuongeza wigo wa ushiriki wa wananchi na wawekezaji katika uwekezaji kupitia masoko ya mitaji.

Mbali na hilo, hatua ya uzinduzi wa mfumo huo pia umelenga kuchochea ukuaji wa sekta ya fedha na uchumi wa wananchi na nchi kwa ujumla ukirahisisha ununuzi na uuzaji wa hisa  hizo kwa njia ya mfumo wa kielektroniki.

Akizindua mfumo huo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA), Nicodemus Mkama amesema ujio wa mfumo huo  unatarajiwa kuleta  matokeo chanya katika sekta jumuishi za kifedha, jambo lililopokelewa vyema na serikali.

“Hii ni baada ya tafiti kuonesha kuwa asilimia 60 ya Watanzania wanatumia huduma za fedha kwa njia ya simu za mkononi, kwetu sisi tunaamini kuwa litakuwa limesaidia  kuunga mkono jitihada mbalimbali za kuyashawishi makundi mbalimbali ya kijamii kujenga utamaduni wa kuwekeza kwenye masoko ya hisa na mitaji,”alisema Mkama.

Awali Ofisa Mtendaji Mkuu wa Soko la Hisa Moremi Marwa, alisema mfumo huo umebuniwa ili kuongeza idadi ya wawekezaji kwenye taasisi hiyo kutoka idadi ya wawekezaji 550,000 waliopo sasa ambao ni sawa na asilimia moja ya watanzania wote na kupata idadi kubwa zaidi katika siku zijazo.

Alisema kuzinduliwa kwa huduma ya Hisa Kiganjani, kutasaidia kuwafikia Watanzania wengi zaidi na hasa waliopo nje ya Jiji la Dar es Salaam na hata  nje ya nchi  ambao hapo awali ilikuwa changamoto  kufikiwa na huduma hizo.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa kuendeleza Sekta ya Fedha Tanzania (FSDT) Sosthenes Kewe, alisema baada ya Tanzania kupata mafanikio ya kuingia uchumi wa kati, hivi sasa inaingia katika uchumi shindani unaohitaji ushiriki mpana wa jamii katika masuala ya kuinua uchumi na kwamba kuanzishwa kwa mfumo wa Hisa Kiganjani unatarajiwa kuchochea harakati hizo.

WAZIRI wa Nishati na Madini, Dk ...

foto
Mwandishi: Oscar Job

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi