loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Tiba iliyomtibu Trump yahidhinishwa

 

TIBA kigamwili ya Covid-19 iliyotumika kumtibu Rais Donald Trump imeidhinishwa na Mdhibiti wa Dawa Marekani kwa ajili ya watu ambao bado hawajalazwa hospitalini kutokana na ugonjwa huo lakini wako katika hatari kubwa.

Mafanikio ya mtengenezaji wa dawa hiyo, Regeneron yalikuja baada ya dawa ya REGEN-COV2 ambayo ni mchanganyiko wa kingamwili mbili zilizotengenezwa maabara, ilionesha kupunguza idadi ya wagonjwa wa Covid-19 kulazwa pamoja na kupunguza idadi ya wagonjwa wenye dalili kwenye vyumba vya dharura.

“Kuidhinisha tiba hizi za kinga ya mwili kunaweza kusaidia wagonjwa wa nje kutolazwa na kupunguza mzigo kwa mfumo wetu wa huduma ya afya,” alisema Kamishna wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (FDA), Stephen Hahn.

Rais na Mkurugenzi Mtendaji wa Regeneron, Leonard Schleifer, alisema kuwa mpango huo ni hatua muhimu katika kupambana na Covid-19 kwa kuwa wagonjwa walio kwenye hatari kubwa nchini humo wanaweza kupata tiba mapema baada ya kuambikizwa.

Matibabu ya kingamwili ya Regeneron ni ya pili kupata idhini ya matumizi ya dharura (EUA) kutoka FDA baada ya tiba kama hiyo iliyotengenezwa na Eli Lilly kupewa idhini Novemba 9 mwaka huu.

RAIS Vladimir Putin wa Urusi na ...

foto
Mwandishi: WASHINGTON, Marekani

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi