loader
Dstv Habarileo  Mobile
Barcelona yazidi  kutaabika La Liga

Barcelona yazidi kutaabika La Liga

ATLETICO Madrid jana ilisogea na kulingana pointi na vinara wa La Liga, Real Sociedad baada ya kuifunga Barcelona ambayo sasa iko nyuma kwa pointi tisa dhidi ya timu mbili za juu kwenye msimamo.

Yannick Carrasco alifunga bao pekee dakika chache kabla ya kwenda mapumziko.

Aidha, Barcelona ilimpoteza beki wake Gerard Pique aliyeumia na kufanya usiku huo wa juzi kuzidi kuwa mbaya kwao.

Pique alionekana kutokuwa sawa na kulazimika kutolewa katika kipindi cha pili.

Barcelona ilithibitisha baada ya mechi hiyo kwamba Pique ameumia goti la mguu wa kulia na kwa sasa anasubiri uchunguzi zaidi.

Hakuna muda wa uhakika kwamba Pique atakuwa nje ya uwanja kwa muda gani pengine anaweza kuwa nje kwa miezi sita.

Ushindi huo umekuwa wa kwanza kwa kocha wa Atletico Madrid, Diego Simeone kwenye La Liga dhidi ya Barcelona katika mechi 18 zilizowakutanisha.

Matokeo hayo yameiacha Barcelona kwenye nafasi ya 10 katika msimamo wa La Liga, wakiwa na pointi 11 katika mechi nane, tisa nyuma ya Sociedad ambayo inaongoza msimamo kwa uwiano mzuri wa mabao dhidi ya Atletico.

Ushindi huu unaifanya Atletico kuwa haijaifungwa kwenye mechi 24 katika michuano yote, huku ni kipigo cha tatu kwa Barca katika mechi nane ilizokwisha cheza.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/893ea2032073e9f649697d0068c8558e.png

“Jesse Lingard atajifunza kutokana na makosa yaliyowapa faida ...

foto
Mwandishi: MADRID, Hispania

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi