loader
Dstv Habarileo  Mobile
Mourinho ampiga  dongo Guardiola

Mourinho ampiga dongo Guardiola

JOSE Mourinho ni kama amempiga dongo kocha wa Manchester City, Pep Guardiola baada ya kumfunga mabao 2-0 kwenye Ligi Kuu juzi.

Mourinho amekisifia kikosi chake cha Tottenham kwamba kilicheza soka safi yenye mbinu nyingi na kuibuka na ushindi.

Spurs ilikuwa kwenye kiwango bora ilipoifunga City mabao 2-0, shukrani kwa mabao kutoka kwa Heung-Min Son na Giovani Lo Celso wakati kikosi cha Mourinho kikilenga mashuti manne pekee langoni mwa City iliyolenga mashuti 22.

Matokeo yalimaanisha Spurs ilimaliza siku ikiwa kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu kwa mara ya kwanza tangu Agosti 2014.

Aliwaambia waandishi wa habari: "Kwa upande wangu, ningependa wachezaji wazungumze zaidi kwa sababu ndio waliokuwa vizuri, walitoa kila kitu, walifuata maelekezo vizuri walifurahisha.”

"Ilikuwa muhimu sana kuiheshimu [City] na bila kusahau timu ilivyo kama tungefuata kile walichokisema watu kuhusu wao kwamba hawako vizuri kama mwanzo ama tungefuata msimamo wa uongo kwa sababu wana mechi moja mkononi, tungecheza tofauti, City ni timu nzuri, kupoteza dhidi ya timu iliyokuwa imejipanga ni vizuri lakini City itabaki kuwa City.

"Hakika unatakiwa kufunga na hatukupata nafasi nyingi, unahitaji kuwa na kipa mzuri kuokoa hatari katika matukio muhimu, lakini tulijua watakuwa zaidi na mpira lakini tungekuwa vizuri zaidi kucheza tulivyocheza kwa sababu tulijua watafanya nini.”

Lakini Mourinho alitoa pongezi maalumu kwa Kane, aliyekuwa mchezaji bora katika mechi hiyo ya juzi na kuongeza pasi ya mabao kufikia tisa baada ya kutoa pasi iliyozaa bao la pili.

"Harry Kane aliwakilisha ari waliyokuwa nayo wachezaji wote, jinsi anavyofanya kazi kwa ajili ya timu ni jinsi ambavyo wote wanafanya,” alisema.
Baada ya mechi hiyo, Tottenham sasa itacheza na Ludogorets kwenye ligi ya Europa ALhamis ya wiki hii kabla ya kuifuata Chelsea mwishoni mwa wiki hii kwenye mechi kabambe ya Ligi Kuu.

Man City itakuwa Olympiakos kwenye Ligi ya Mabingwa keshokutwa kabla  ya kuikaribisha Burnley kwenye Ligi Kuu mwishoni mwa wiki hii.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/6671585d772c247e712d38b62662b25e.jpg

“Jesse Lingard atajifunza kutokana na makosa yaliyowapa faida ...

foto
Mwandishi: LONDON, England

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi