loader
Dstv Habarileo  Mobile
Nicki Minaj asherehekea miaka 10 ya albamu

Nicki Minaj asherehekea miaka 10 ya albamu

RAPA Onika Maraj-Petty 'Nicki Minaj' jana alitarajia kufanya sherehe ya kuadhimisha  miaka 10 ya albumu yake ya 'Pink Friday', aliyoiachia mwaka 2010.

Pink Friday ndiyo album ya Nicki Minaj iliyouza zaidi kuliko album zake zingine ambayo Staa huyo wa kike aliuza nakala milioni 3 hadi sasa.

Minaj ameongeza ngoma nyingine nakuifanya albumu hiyo kufikisha nyimbo 21 ikiwa ni pamoja na wimbo wake uliopewa jina la Roman Revenge ambao sasa amemshirikisha Rapa Lil wayne, kwani Awali alimshirikisha Eminem.

"Ni albamu yenye mafanikio makubwa kwenye maisha yangu ya kimuziki na sio ajabu kufanya tukio kama hili la kusherekea na kushukuru lakini pia nawapongeza mashabiki zangu kwani nimeuza nakala nyingi duniani kote,"alisema Minaj.

Alisema tangu alipoachia albamu hiyo, inafikia miaka 10 na bado kwenye soko la muziki inafanya vyema kwa nyimbo zinazounda kupendwa zaidi kusikilizwa.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/c07fe351551edd9d03a46af127f39df4.jpg

“Jesse Lingard atajifunza kutokana na makosa yaliyowapa faida ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi