loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

 Waathirika Dawa za Kulevya wakataa unyanyapaa

Wito umetolewa kwa jamii kutowanyanyapaa  waathirika wa Dawa za Kulevya walioamua kuachana na matumizi ya dawa hizo kwa kuwaona kama watu wasioaminika.

Waathirika wa dawa za kulevya wanaotibiwa kwenye kituo cha Pedderef kilichopo Kigamboni, Dar es Salaam wametoa wito huo walipokuwa wanapokea msaada wa vyakula na mahitaji mbalimbali vilivyotolewa na kampuni ya michezo ya kubahatisha ya Meridian Bet.

Akizungumza katika tukio hilo mmiliki wa kituo hicho, Nuru Salehe amesema kuwa waathirika wa dawa hizo wamekuwa wanakumbana na changamoto kubwa ya kunyanyapaliwa hata baada ya kutoka soba.

Aidha, Salehe ambaye aliwahi kuwa muathirika wa matumizi wa dawa hizo amesema kuwa  “ jamii inapaswa kupewa elimu juu ya tatizo hili kwani ni ugonjwa kama magonjwa mengine,lakini kuna changamoto muathirika anapoamua kuacha na kuomba kusaidiwa   kurudi shule au mtaji wa kuanzisha biashara jamii mara nyingi inakuwa haimuelewi”.

Amesema changamoto hizo ndio zinapelekea wengi wao kurudia matumizi ya dawa hizo wakiamini ndio njia sahihi ya kujipatia faraja wakati kiualisia ndio wanakuwa  wanaongeza ukubwa wa tatizo.

 

 

 

NAIBU Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, ...

foto
Mwandishi: Na Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi