loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wizara ya Kilimo Kushirikiana na JKT kuzalisha mbegu

Katika  kuhakikisha inawawezesha wakulima   kupata miche bora ya Kahawa, Wizara ya Kilimo  imepanga kuingia makubaliano na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) ili kutumia ardhi yake kuzalisha mbegu za zao hilo kwa lengo la kukidhi mahitaji ya wakulima.

 Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo,Gerald Kusaya alipofanya ziara ya kukagua shamba la kahawa lenye ukubwa wa ekari 50 katika kambi ya 822 JKT Kiteule cha Tarime mkoani mara.

“Wizara ya Kilimo ipo tayari kuingia makubaliano na JKT kuzalisha miche bora mingi ya Kahawa ili kutosheleza mahitaji ya wakulima wa mkoa wa Mara na mikoa jirani na kwa kuanza tutatoa shilingi milioni 19 ili Taasisi ya Utafiti wa Zao la Kahawa (TACRI) waanzishe kitalu cha miche humu kambini” amesema Kusaya.

 Aidha, Kusaya ameliagiza Jeshi la Kujenga Taifa kutumia fursa iliyopatikana nchini Misri ya kuzalisha mahindi ya njano ambayo yanahitajika kwa kiwango cha tani 25,000 kwa mwezi ifikiapo Julai mwakani  kwakuwa wataalam na uwezo wanao.

Kwa upande wake Kaimu Kamanda Kikosi cha 822 KJ Kiteule cha Tarime Meja MM Kinana amemweleza  Kusaya kuwa tayari katika msimu wa 2020/21  wamefanikiwa kupanda ekari 52 za kahawa na mahindi  huku lengo likiwa kufikia    ekari 200.

NAIBU Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, ...

foto
Mwandishi: ALFRED LUKONGE

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi