loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Pinda ashauri upandaji miti kwa wingi

WAZIRI Mkuu mstaafu, Mizengo Pinda amewashauri watendaji katika halmashauri zote nchini kuhakikisha miti milioni 1.5 inapandwa kila mwaka ili kupambana na madhara ya mabadiliko ya tabia nchi.

Pinda aliyasema hayo katika Shule ya Sekondari Msanga, wilayani Chamwino, mkoani Dodoma wakati wa upandaji miti uliloandaliwa na taasisi ya habari ya Habari Development Association (HDA). Lengo lake ni kuikijanisha Dodoma na kurudisha uoto wake wa asili.

Alisema katika kuhakikisha nchi inapambana na madhara ya mabadiliko ya tabia nchi, Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) imeelekeza suala la upandaji miti katika kila halmashauri kuwa ni miti milioni 1.5 kila mwaka.

"Kwa miaka mitano ya uongozi wa Serikali ya Awamu ya Tano imepata mafanikio ambapo zaidi ya miti milioni 608 imepandwa nchini,” alisema.

Pia aliitaka jamii kuacha tabia ya kuchoma misitu hovyo huku akiwatahadharisha wavutaji sigara wanaotupa hovyo vipisi vyenye moto, kuacha tabia hiyo.

Aliushauri uongozi wa shule hiyo na wananchi kutunza miti hiyo kwa kuimwagilia maji ili imee vizuri na kufikia lengo lililokusudiwa.

Pia aliitaka jamii kuhakikisha wajawazito wanakula vyakula vya jamii ya mbogamboga na matunda ili kuwanusuru kupata watoto wenye utapiamlo.

"Katika zoezi hili la kukijanisha Dodoma tuwafundishe watoto kupanda miti hasa ya matunda kwa sababu miili ya binadamu inahitaji sana chakula cha matunda na mbogamboga lakini pia kwa sababu Tanzania tunakabiliwa na utapiamlo kwa kuwa hatuli vyakula hivyo ambavyo hupambana na tatizo la udumavu," alisema.

Kwa mujibu wa Pinda, watoto milioni tatu waliodumaa wapo nchini na hali hii inatokana na mama zao kutokula vyakula vinavyostahili hasa mbogamboga na matunda wakati wakiwa wajawazito."

Awali, Katibu wa HAD, Godfrey Mbowe alisema taasisi hiyo imekusudia kupanda miti 5,000 katika kijiji hicho na kwamba mpango wao ni hadi kufikia mwaka 2021 wawe wamepanda miti 100,000 katika Mkoa wa Dodoma.

NAIBU Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, ...

foto
Mwandishi: Anastazia Anyimike

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi