loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Uswisi yatoa bil 19/- mradi misitu ya vijiji

SERIKALI ya Uswisi kupitia Shirika la Maendeleo la nchi hiyo (SDC), kwa nyakati tofauti imetoa Sh bilioni 19 kutekeleza mradi wa uhifadhi shirikishi wa misitu ya vijiji  unaotarajiwa kumalizika mwaka 2023.

Mkurugenzi wa Shirika la Kuhifadhi Misitu ya Asili Tanzania (TFCG), Charles Meshack alisema hayo katika Kijiji cha Mahenge, wilayani Kilolo, mkoani Iringa.

Meshack alisema kipindi cha miaka sita cha awamu ya kwanza na ya pili SDC ilitoa zaidi ya Sh bilioni 12 kwa ajili ya mradi huo na katika awamu ya tatu inayotarajiwa kukamilika mwaka 2023, imetoa Sh bilioni saba kutekeleza mradi huo.

"Awamu ya tatu imejikita katika kujengea uwezo wilaya zingine kuanzisha usimamizi shirikishi wa misitu na zimeongezwa wilaya nne ili nazo ziweze kuambukiza wilaya nyingine na hivyo kuwezesha mbinu hiyo kusambaa hatua kwa hatu hadi kufikia nchi nzima," alisema Meshack.

Alisema Tanzania ina jumla ya hekta milioni 48.1 za misitu na milioni 22 kati ya hizo sawa na asilimia 45 ipo chini ya ardhi za vijiji.

"Lakini kwa sasa iliyohifadhiwa chini ya usimamizi shirikishi wa misitu ni asilimia tano (5) wakati hekta milioni 17 na zisiposimiwa zinaweza kutoweka," alisema  Meshack.

Mwakilishi wa Balozi wa Uswisi nchini Tanzania, Peter Selder, alisema ubalozi huo  nchini kupitia SDC umeahidi kuendeleza ushirikiano na Serikali ya Tanzania na wadau wengine katika uhifadhi shirikishi wa misitu.

Selder alikuwa kwenye Kijiji cha Mahenge kwa ziara ya wajumbe wa Bodi ya Ushauri wa Mradi wa Uhifadhi Shirikishi wa Misitu ya Vijiji kuona maendeleo na ushiriki wa wanakijiji katika jitihada za kulinda misitu na kunufaika na rasilimali zinazotokana na uhifadhi huo.

Selder alisema ameridhishwa na mbinu inayotumiwa na TFCG na Mtandao wa Jamii wa Usimamizi wa Misitu (Mjumita) kuijengea uwezo jamii, viongozi na wadau wengine kuhusu namna ya kuilinda, kuihifadhi na kunufaika na mazao ya misitu.

Mkurugenzi wa Mjumita, Rahma Njaidi alisema misitu mingi inaangamia pengine kwa kuwa jamii haifahamu thamani na faida za misitu hiyo.

"Kuna vijiji vingi nchi hii ambavyo vina misitu ya miyombo lakini bahati hii imewaangukia nyinyi watu wa Kijiji cha Mahenge Wilaya ya Kilolo, hii ni fursa kwenu kuhifadhi na kunufaika na matunda ya uhifadhi shirikishi wa misitu hivyo muwasikilize wataalamu ili muweze kufanikiwa kama wenzenu," alisema Rahma.

Mradi wa Usimamizi Shirikishi wa Misitu ya Jamiii (USMJ) inatekelezwa kupitia mradi wa kuleta Mageuzi katika Sekta ya Mkaa Tanzania (TTCS) na mradi wa kuhifadhi Misitu kwa kuwezesha Biashara Endelevu ya Misitu (CoFOREAT) kwa ufadhili wa SDC.

Katibu wa Shirikisho la Vyama vya Tiba Asili ...

foto
Mwandishi: John Nditi, Morogoro

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi