loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Fifa yamtia kitanzi Rais wa Caf

SHIRIKISHO la soka la kimataifa, Fifa, limemfungia miaka mitano Rais wa Shirikisho la Soka Afrika, Caf, Ahmad Ahmad kwa matumizi mabaya ya fedha.

Rais huyo wa Caf mwenye umri wa miaka 60 amekutwa na hatia ya kutumia vibaya fedha kwa kutoa ofa na zawadi mbalimbali.

"Uchunguzi juu yake umefanywa kwa muda mrefu na ilianza baada ya kuingia madarakani 2017-2019, kuna uvunjifu mkubwa wa sheria na matumizi ya fedha ikiwamo kupeleka watu Umrah na Macca,” ilisema taarifa ya Fifa jana.
Mbali na kifungo hicho,  Ahmad pia ametozwa faini ya dola za Marekani 200,000.

Raia huyo wa Madagascar anaweza kukata rufaa kupinga hukumu hiyo katika Mahakama ya Michezo ya Kimataifa, CAS, ndani ya siku 60 baada ya kupata barua yake ya hukumu.
Mwezi uliopita, Ahmad Rais wa zamani wa chama cha soka cha Madagascar alitangaza kugombea tena kipindi cha pili katika uchaguzi mkuu wa Caf unaotarajiwa kufanyika Machi mwakani.

Jambo hilo linazusha mashaka kama Ahmad aliyechaguliwa Rais wa Caf mwaka 2017 atakuwa na sifa ya kuendelea kugombea kama atakata rufaa na kushindwa.

Nafasi yoyote tete ya kugombea itategemea na maamuzi ya rufaa yake atakayoikata CAS kama atashinda, lakini si tu kushinda bali uharaka wa kusikilizwa ili kuthibitika kama anaweza kuwa mgombea tena.

Ahmad kwa siku za karibuni alipumzika kuongoza Caf kwa madai ya kushughulikia afya yake na nafasi yake kumuachia makamu wake Constant Omari kuongoza Shirikisho hilo.

BERNARD Morrison ameng’ara baada ya kuifungia timu yake mabao mawili ...

foto
Mwandishi: BERN, Uswisi

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi