loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

RC KUNENGE AWAPONGEZA WAUGUZI DAR ES SALAAM

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Aboubakar Kunenge amewapongeza Wauguzi wa Mkoa huo kwa kazi nzuri wanayoifanya ya kuokoa maisha ya wananchi jambo lililosaidia kupunguza vifo.

RC Kunenge amezungumza hayo leo wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wauguzi Mkoa wa Dar es salaam na kuwahimiza kuchapa kazi na kuwaahidi kuwa Serikali itaendelea kushirikiana nao.

Amesema Serikali imekuwa ikifanya kazi kubwa ya kuboresha huduma za Afya kupitia Ujenzi wa hospitali, Zahanati, Vituo vya Afya na kununua Vifaa tiba ili kuhakikisha wanatatua kero za wananchi.

Mganga Mkuu wa Mkoa huo Dr Rashid Mfaume ametoa wito kwa wananchi kujitokeza kwenye Viwanja vya Karimjee kujionea kazi zinazofanywa na Wauguzi wa Mkoa huo.

Katibu wa Shirikisho la Vyama vya Tiba Asili ...

foto
Mwandishi: Rahimu Fadhili

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi